Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 1 · Art. 1

Mamlaka ya wananchi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu
kulingana na Katiba hii.
(2) Wananchi watatekeleza mamlaka yao kwa njia ya moja kwa moja au kupitia
kwawawakilishi wao waliochaguliwa kidemokrasia.
(3) Mamlaka ya wananchi katika Katiba hii yamepewa idara zifuatazo za Serikali,
ambazo zitatekeleza majukumu yao kulingana na Katiba hii –
  (a) Bunge na mabaraza ya kutunga sheria katika Serikali za Kaunti;
  (b) Serikali ya kitaifa na mifumo ya Serikali za Kaunti; na
  (c) Idara ya mahakama na tume zingine huru ;
(4) mamlaka ya wananchi yanatekelezwa katika-
  (a) kiwango cha kitaifa; na
  (b) kiwango cha kaunti.
Kwa maneno rahisi
  • Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya.
    Art. 1(1)

    (1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.

    Soma kifungu kamili →
  • Wananchi hutumia mamlaka yao moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa.
    Art. 1(2)

    (2) Wananchi watatekeleza mamlaka yao kwa njia ya moja kwa moja au kupitia kwawawakilishi wao waliochaguliwa kidemokrasia.

    Soma kifungu kamili →
  • Mamlaka yanatekelezwa katika ngazi ya kitaifa na ya kaunti.
    Art. 1(4)

    (4) mamlaka ya wananchi yanatekelezwa katika- (a) kiwango cha kitaifa; na (b) kiwango cha kaunti.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Nchi ni ya wananchi. Viongozi wana mamlaka kwa sababu wananchi wanawapa.
    Art. 1(1)

    (1) Mamlaka yote makuu ni ya wananchi wa Kenya na yanaweza kutekelezwa tu kulingana na Katiba hii.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →