Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 2 · Art. 10

Maadili ya kitaifa na kanuni za utawala

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Maadili ya kitaifa, kanuni na malengo yaliyo katika Sura hii yatazingatiwa na idara
mbalimbali za Serikali, watumishi wa umma na watu wote wanapo –
  (a) tekeleza au kufasiri Katiba hii;
  (b) tumia, tekeleza au kufasiri sheria yoyote; au
  (c) tunga, au kutekeleza maamuzi kuhusu sera ya kitaifa.
(2) Maadili ya kanuni za uongozi ni pamoja na –
  (a) Uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa
  sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu;
  (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu,
  kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa.
  (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na
  (d) maendeleo endelevu.
Kwa maneno rahisi
  • Maadili ya kitaifa yanabana vyombo vyote vya Serikali na maafisa wa umma wanapotumia Katiba, kutunga sheria au kufanya maamuzi ya sera.
    Art. 10(1)

    (1) Maadili ya kitaifa, kanuni na malengo yaliyo katika Sura hii yatazingatiwa na idara mbalimbali za Serikali, watumishi wa umma na watu wote wanapo – (a) tekeleza au kufasiri Katiba hii; (b) tumia, tekeleza au kufasiri sheria yoyote; au (c) tunga, au kutekeleza maamuzi kuhusu sera ya kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Maadili hayo ni pamoja na uzalendo, umoja wa kitaifa, utawala wa sheria, demokrasia na ushiriki wa wananchi.
    Art. 10(2)(a)

    (a) Uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu;

    Soma kifungu kamili →
  • Pia ni pamoja na hadhi ya binadamu, usawa, haki za kijamii, kutobagua na kulinda waliotengwa.
    Art. 10(2)(b)

    (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu, kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Ni pamoja na utawala bora, uadilifu, uwazi na uwajibikaji.
    Art. 10(2)(c)

    (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Viongozi lazima wawe wa haki, waaminifu na wawajumuishe wote wanapofanya maamuzi.
    Art. 10(2)

    (2) Maadili ya kanuni za uongozi ni pamoja na – (a) Uzalendo, umoja wa kitaifa, kushirikiana na ugatuzi wa mamlaka, utawala wa sheria, demokrasia na kushiriki kwa watu; (b) heshima ya binadamu, usawa, haki za jamii, kushirikishwa, haki za binadamu, kutobagua na kulindwa kwa makundi yaliyotengwa. (c) utawala mwema, uadilifu, uwazi na uwajibikaji; na (d) maendeleo endelevu.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →