Sura 2 · Art. 11
Utamaduni
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Katiba hii inatambua utamaduni kama msingi wa taifa na jumla ya ustaarabu wa watu na taifa la Kenya. (2) Serikali– (a) itakuza aina zote za kitaifa na kitamaduni za kujieleza kupitia fasihi, sanaa, sherehe za kitamaduni, sayansi, mawasiliano, habari, vyombo vya habari, uchapishaji, maktaba na turathi nyingine za kitamaduni; (b) itatambua jukumu la sayansi na teknolojia za kiasili katika maendeleo ya nchi; (c) itatambua haki za kiubunifu za watu wa Kenya; (3) Bunge litatunga sheria- (a) kuhakikisha kwamba jamii zinapewa fidia au mrabaha kwa kutumiwa kwa turathi zao za kitamaduni; na (b) kutambua na kulinda umiliki wa mbegu na mimea mbalimbali ya kiasili, sifa tofauti za kimaumbile na matumizi yake miongoni mwa jamii za Kenya.
Kwa maneno rahisi
- Katiba inatambua utamaduni kama msingi wa taifa.
Art. 11(1)
(1) Katiba hii inatambua utamaduni kama msingi wa taifa na jumla ya ustaarabu wa watu na taifa la Kenya.
Soma kifungu kamili → - Serikali lazima ikuze usemi wa kitamaduni, sayansi na teknolojia za kienyeji.
Art. 11(2)
(2) Serikali– (a) itakuza aina zote za kitaifa na kitamaduni za kujieleza kupitia fasihi, sanaa, sherehe za kitamaduni, sayansi, mawasiliano, habari, vyombo vya habari, uchapishaji, maktaba na turathi nyingine za kitamaduni; (b) itatambua jukumu la sayansi na teknolojia za kiasili katika maendeleo ya nchi; (c) itatambua haki za kiubunifu za watu wa Kenya;
Soma kifungu kamili → - Jamii lazima zipate fidia au mrahaba kwa matumizi ya tamaduni na urithi wao wa kitamaduni.
Art. 11(3)(a)
(a) kuhakikisha kwamba jamii zinapewa fidia au mrabaha kwa kutumiwa kwa turathi zao za kitamaduni; na
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Tamaduni zetu ni muhimu, na serikali lazima izikuze na kuzilinda.
Art. 11(1)
(1) Katiba hii inatambua utamaduni kama msingi wa taifa na jumla ya ustaarabu wa watu na taifa la Kenya.
Soma kifungu kamili →