Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 3 · Art. 15

Uraia kwa kujiandikisha

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mtu ambaye ameolewa na raia kwa muda wa angalau miaka saba ana haki, kutuma
maombi ya kusajiliwa kama raia.
(2) Mtu ambaye amekuwa mkazi halali nchini Kenya kwa muda wa miaka saba
mfululizo, na ambaye anatimiza masharti yote ya sheria yaliyoidhinishwa na Bunge,
anaweza kutuma maombi ya kujiandikisha kama raia.
(3) Mtoto ambaye si raia na ambaye ni wa kupangwa na raia, ana haki ya kuwa raia kwa
kutuma maombi .
(4) Bunge litatunga sheria itakayotoa masharti ambayo yatazingatiwa kuwapa uraia watu
binafsi ambao ni raia wa nchi nyingine.
(5) Kifungu hiki kitatumika kwa mtu kuanzia tarehe ya kuanza kutumiwa kwa Katiba
hii , lakini mahitaji yoyote ambayo ni lazima yatimizwe kabla ya mtu anayestahili
kusajiliwa kama raia, yatachukuliwa kama yaliyotimizwa pasi na kuzingatia iwapo
mtu huyu aliyatimiza kabla au baada ya tarehe ya kuanza kutekelezwa kwa Katiba
hii, au kwa kiwango fulani kabla au baada ya tarehe ya kutekelezwa.
Kwa maneno rahisi
  • Mtu aliyeolewa na raia kwa angalau miaka saba anaweza kuomba kujiandikisha kama raia.
    Art. 15(1)

    (1) Mtu ambaye ameolewa na raia kwa muda wa angalau miaka saba ana haki, kutuma maombi ya kusajiliwa kama raia.

    Soma kifungu kamili →
  • Mtu anayeishi Kenya kihalali kwa angalau miaka saba mfululizo anaweza kuomba kujiandikisha kama raia.
    Art. 15(2)

    (2) Mtu ambaye amekuwa mkazi halali nchini Kenya kwa muda wa miaka saba mfululizo, na ambaye anatimiza masharti yote ya sheria yaliyoidhinishwa na Bunge, anaweza kutuma maombi ya kujiandikisha kama raia.

    Soma kifungu kamili →
  • Mtoto ambaye si raia lakini amelelewa na raia anaweza kuomba kujiandikisha kama raia.
    Art. 15(3)

    (3) Mtoto ambaye si raia na ambaye ni wa kupangwa na raia, ana haki ya kuwa raia kwa kutuma maombi .

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Watu wanaooa au kuolewa na Mkenya au wanaoishi Kenya kwa miaka mingi wanaweza kuomba kuwa raia wa Kenya.
    Art. 15(2)

    (2) Mtu ambaye amekuwa mkazi halali nchini Kenya kwa muda wa miaka saba mfululizo, na ambaye anatimiza masharti yote ya sheria yaliyoidhinishwa na Bunge, anaweza kutuma maombi ya kujiandikisha kama raia.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →