Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 3 · Art. 17

Kupokonywa uraia

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Iwapo mtu amepata uraia kwa kusajiliwa, uraia huo unaweza kupokonywa iwapo-
  (a) mtu huyo alijipatia uraia huo kwa njia ya ulaghai, udanganyifu wa uwakilishi au
  kuficha ukweli unaotakikana;
  (b) iwapo mtu huyo, katika vita vyovyote ambavyo Kenya ilihusika, kinyume na sheria
  alifanya biashara au kuwasiliana na adui au amejihusisha au kushiriki biashara na
  ambayo kwa kujua, ilitekelezwa kwa namna ambayo ilikuwa ni kusaidia adui;
  (c) katika kipindi cha miaka mitano baada ya kusajiliwa, amepatikana na hatia na
  kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu au zaidi; au
  (d) wakati wowote ule baada ya kusajiliwa amepatikana na hatia ya uhaini au hatia
  ambayo-
  (i) amepewa adhabu ya kifungo cha angalau miaka saba au zaidi; au
  (ii) hukumu kali zaidi inaweza kutolewa.
(2) Uraia wa mtu ambaye alichukuliwa kuwa raia kwa kuzaliwa kama inavyofikiriwa
katika Kifungu cha 14 (4) unaweza kupokonywa iwapo-
  (a) uraia ulipatikana kwa njia ya ulaghai, udanganyifu wa uwakilishi au kuficha
  ukweli unaotakikana kwa mtu yoyote;
  (b) utaifa au kuzaliwa kwa mtu huyo kunajulikana na kufichua kwamba mtu huyo
  alikuwa raia wa nchi nyingine; au
  (c) umri wa mtu huyo unakuja kujulikana na kufichua kwamba alikuwa na umri wa
  zaidi ya miaka minane alipopatikana nchini Kenya.
Kwa maneno rahisi
  • Uraia uliopatikana kwa kujiandikisha unaweza kupokonywa kama ulipatikana kwa udanganyifu au uwakilishi wa uongo.
    Art. 17(1)(a)

    (a) mtu huyo alijipatia uraia huo kwa njia ya ulaghai, udanganyifu wa uwakilishi au kuficha ukweli unaotakikana;

    Soma kifungu kamili →
  • Uraia uliodhaniwa kwa mtoto aliyepatikana unaweza kupokonywa kama utaifa au wazazi wake wanajulikana na kudhihirisha kuwa ni raia wa nchi nyingine.
    Art. 17(2)(b)

    (b) utaifa au kuzaliwa kwa mtu huyo kunajulikana na kufichua kwamba mtu huyo alikuwa raia wa nchi nyingine; au

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama mtu alipata uraia wa Kenya kwa kusema uongo, unaweza kuondolewa.
    Art. 17(1)(a)

    (a) mtu huyo alijipatia uraia huo kwa njia ya ulaghai, udanganyifu wa uwakilishi au kuficha ukweli unaotakikana;

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →