Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 1 · Art. 22

Utekelezaji wa Sheria ya Haki

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani akidai kunyimwa, kukiukwa, au
kutishiwa haki au uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki
(2) Pamoja na kuwasilishwa na mtu anayewawakilisha, kesi chini ya ibara ya (1)
inaweza kuwasilishwa mahakamani na-
  (a) mtu anayemwakilisha mtu mwingine asiyeweza kujiwakilisha;
  (b) mtu ambaye pia ni mwanachama wa kundi fulani au kwa hiari ya kundi au tabaka
  fulani la watu;
  (c) mtu aliyejitolea kwa niaba ya umma; na
  (d) muungano uliojitolea kwa niaba ya mtu mmoja au kundi miongoni mwa wanachama.
(3) Jaji Mkuu ataweka kanuni zinazoruhusu kesi zilizotajwa katika kifungu hiki ambazo
zitaridhisha kigezo kwamba-
  (a) haki za kulalamika zilizotolewa katika ibara ya (2) zinatekelezwa kwa ukamilifu;
  (b) urasmi unaohusiana na kesi hizo, kukiwemo kuanzishwa kwa kesi, unawekwa
  kwa kiwango cha chini, na hasa pakiwa na haja, mahakama itakubali kuwepo kwa
  kesi kwa misingi ya rekodi zisizo na ulazima wa urasmi;
  (a) hakuna fedha zitakazotozwa kwa kuanzisha kesi;
  (b) mahakama, kwa kuzingatia kanuni za haki za kimsingi haitazuiwa bila sababu na
  mahitaji madogo madogo; na
  (c) shirika au mtu binafsi mwenye ujuzi maalum anaweza, kwa idhini ya mahakama,
  kujitokeza kama rafiki wa mahakama.
(4) Kukosekana kwa kanuni zinazoangaziwa katika ibara ya (3) hakutamnyima
yeyote haki ya kuwasilisha malalamiko kulingana na Kifungu hiki, kusikizwa
kwa malalamiko hayo na kuamriwa na mahakama.
Kwa maneno rahisi
  • Kama haki zako zinakataliwa au zinatishiwa, unaweza kwenda mahakamani.
    Art. 22(1)

    (1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani akidai kunyimwa, kukiukwa, au kutishiwa haki au uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki

    Soma kifungu kamili →
  • Mtu anaweza kwenda mahakamani kwa niaba ya mtu mwingine, kikundi, maslahi ya umma, au chama.
    Art. 22(2)

    (2) Pamoja na kuwasilishwa na mtu anayewawakilisha, kesi chini ya ibara ya (1) inaweza kuwasilishwa mahakamani na- (a) mtu anayemwakilisha mtu mwingine asiyeweza kujiwakilisha; (b) mtu ambaye pia ni mwanachama wa kundi fulani au kwa hiari ya kundi au tabaka fulani la watu; (c) mtu aliyejitolea kwa niaba ya umma; na (d) muungano uliojitolea kwa niaba ya mtu mmoja au kundi miongoni mwa wanachama.

    Soma kifungu kamili →
  • Hakuna ada inayotozwa kwa kuanzisha kesi hizi za mahakama.
    Art. 22(3)(c)

    (c) shirika au mtu binafsi mwenye ujuzi maalum anaweza, kwa idhini ya mahakama, kujitokeza kama rafiki wa mahakama.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama mtu anakutenda isivyo haki na kuondoa haki zako, unaweza kuomba mahakama ikusaidie.
    Art. 22(1)

    (1) Kila mtu ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani akidai kunyimwa, kukiukwa, au kutishiwa haki au uhuru wa kimsingi ulioko katika Sheria ya Haki

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →