Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 1 · Art. 24

Mipaka ya haki au uhuru wa kimsingi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Haki ya uhuru wa kimsingi iliyo katika Sheria ya Haki haiwezi kuwekewa mipaka
isipokuwa kupitia kwa sheria na iwe tu kwamba mipaka ina maana, na ni ya haki
katika jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia, na chini ya misingi ya heshima ya
binandamu, usawa na uhuru, na kwa kuzingatia vipengele muhimu vikiwemo-
  (a) hali ya haki hiyo au uhuru wa kimsingi;
  (b) umuhimu wa lengo la mipaka hiyo;
  (c) hali na kiwango cha mipaka hiyo;
  (d) haja ya kuhakikisha kuwa kufurahia wa haki hizo na uhuru huo wa kibinafsi kwa
  mtu yeyote hautatizi haki na uhuru wa kimsingi wa watu wengine; na
  (e) uhusiano uliopo kati ya mpaka na lengo lake na endapo kuna njia zingine
  zisizotatiza za kufikia lengo hilo.
(2) Licha ya ibara ya (2), sharti la sheria linalowekea mipaka haki au uhuru wa
kimsingi-
  (a) ikiwa ni sharti lililotungwa au kurekebishwa kabla au baada ya siku ya
  kuanza kutumika Katiba hii, si halali, isipokuwa sheria hiyo haswa inadhihirisha
  madhumuni ya kuiwekea mipaka haki hiyo au uhuru wa kimsingi na kiwango cha
  mipaka hiyo;
  (b) halitachukuliwa kama kuzuia haki au uhuru uliotajwa katika Sheria ya Haki
  isipokuwa pale ambapo sharti hilo linaeleza wazi na kwa yakini kuhusu haki au
  uhuru wa kimsingi unaopaswa kuzuiwa na hali au kiwango cha mipaka hiyo; na
  (c) halitazuia haki au uhuru wa kimsingi unaotajwa katika Sheria ya Haki ili
  kupunguza uzito na umuhimu uliowekwa katika haki hiyo.
(3) Serikali au mtu anayetaka kuhalalisha mpaka fulani atapaswa kuthibitishia
mahakama, mahakama maalum au mamlaka nyingine kuwa mahitaji ya Kifungu hiki
yameridhishwa.
(4) Masharti katika Sura hii kuhusu usawa yatatumika kwa wote ila tu pale ambapo
patahitajika utekelezaji wa Sheria ya Kiislamu mbele ya mahakama za Kadhi kwa
waumini wa Kiislamu kwa mujibu wa hadhi zao za kibinafsi, hali ya ndoa, talaka na
urithi.
(5) Licha ya ibara za (1) na (2), sharti la sheria linaweza kuwekea mipaka utekelezaji
wa haki na/au uhuru wa kimsingi katika masharti kwa watu wanaohudumu katika
Vikosi vya Usalama vya Kenya, au Huduma za Polisi za Kitaifa-
  (a) Kifungu cha 31- Faragha;
  (b) Kifungu cha 36 -Uhuru wa kutangamana
  (c) Kifungu cha 37- Mikutano, maandamano, migomo na malalamiko;
  (d) Kifungu cha 41 –Mahusiano ya kikazi;
  (e) Kifungu cha 43 – Haki za kiuchumi na kijamii;
  (f) Kifungu cha 49 –Haki za watu waliotiwa mbaroni;
Kwa maneno rahisi
  • Haki inaweza kuwekewa mipaka kwa sheria tu, na tu pale mpaka huo unapokuwa wa haki na unastahili katika jamii huru na ya kidemokrasia.
    Art. 24(1)

    (1) Haki ya uhuru wa kimsingi iliyo katika Sheria ya Haki haiwezi kuwekewa mipaka isipokuwa kupitia kwa sheria na iwe tu kwamba mipaka ina maana, na ni ya haki katika jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia, na chini ya misingi ya heshima ya binandamu, usawa na uhuru, na kwa kuzingatia vipengele muhimu vikiwemo- (a) hali ya haki hiyo au uhuru wa kimsingi; (b) umuhimu wa lengo la mipaka hiyo; (c) hali na kiwango cha mipaka hiyo; (d) haja ya kuhakikisha kuwa kufurahia wa haki hizo na uhuru huo wa kibinafsi kwa mtu yeyote hautatizi haki na uhuru wa kimsingi wa watu wengine; na (e) uhusiano uliopo kati ya mpaka na lengo lake na endapo kuna njia zingine zisizotatiza za kufikia lengo hilo.

    Soma kifungu kamili →
  • Hata ukiwekewa mpaka, haki haiwezi kuondolewa maana yake ya msingi.
    Art. 24(2)(c)

    (c) halitazuia haki au uhuru wa kimsingi unaotajwa katika Sheria ya Haki ili kupunguza uzito na umuhimu uliowekwa katika haki hiyo.

    Soma kifungu kamili →
  • Serikali lazima iweze kuonyesha mahakamani kwamba mpaka wowote wa haki unastahili.
    Art. 24(3)

    (3) Serikali au mtu anayetaka kuhalalisha mpaka fulani atapaswa kuthibitishia mahakama, mahakama maalum au mamlaka nyingine kuwa mahitaji ya Kifungu hiki yameridhishwa.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kanuni zingine zinaweza kuweka mpaka kwa haki, lakini tu kama ni za haki na zinahitajika kulinda wengine.
    Art. 24(1)

    (1) Haki ya uhuru wa kimsingi iliyo katika Sheria ya Haki haiwezi kuwekewa mipaka isipokuwa kupitia kwa sheria na iwe tu kwamba mipaka ina maana, na ni ya haki katika jamii iliyo wazi na ya kidemokrasia, na chini ya misingi ya heshima ya binandamu, usawa na uhuru, na kwa kuzingatia vipengele muhimu vikiwemo- (a) hali ya haki hiyo au uhuru wa kimsingi; (b) umuhimu wa lengo la mipaka hiyo; (c) hali na kiwango cha mipaka hiyo; (d) haja ya kuhakikisha kuwa kufurahia wa haki hizo na uhuru huo wa kibinafsi kwa mtu yeyote hautatizi haki na uhuru wa kimsingi wa watu wengine; na (e) uhusiano uliopo kati ya mpaka na lengo lake na endapo kuna njia zingine zisizotatiza za kufikia lengo hilo.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →