Sura 4, Sehemu 2 · Art. 27
Usawa na Uhuru dhidi ya kubaguliwa
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na kupata manufaa sawa ya sheria. (2) Usawa unajumuisha kupata haki na uhuru wote wa kimsingi kwa njia iliyo kamili na sawa. (3) Wanawake na wanaume wana haki ya usawa ikiwemo haki ya kupata nafasi sawa katika shughuli za kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii. (4) Serikali, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, haitakuwa na ubaguzi dhidi ya mtu yeyote kwa misingi yoyote ikiwemo asili, jinsia, ujauzito, hali ya mtu kindoa, hali ya kiafya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa. (5) Mtu hatakuwa na ubaguzi dhidi ya mwingine kwa njia ya moja kwa moja au vinginevyo katika misingi iliyotajwa na kuonyeshwa na ibara ya (4). (6) Ili kutoa athari kamilifu za kutimiza haki zinazohakikishiwa na Kifungu hiki, Serikali itachukua hatua za kisheria na nyinginezo kukiwemo vitendo sawazishi na sera ambazo zimebuniwa kupinga athari za kutonufaika kwa watu binafsi au makundi ya watu kwa sababu ya ubaguzi wa hapo awali. (7) Hatua yoyote inayochukuliwa chini ya ibara ya (6) itashughulikia kikamilifu fidia yoyote kwa kuzingatia uhitaji ulioko . (8) Pamoja na hatua zinazokusudiwa katika ibara ya (6), Serikali itachukua hatua za kisheria na nyinginezo ili kutekeleza kanuni kwamba, idadi ya watu waliochaguliwa au kuteuliwa katika mashirika haitakuwa na wanachama zaidi ya thuluthi mbili wa jinsia moja.
Kwa maneno rahisi
- Kila mtu ni sawa mbele ya sheria, na kila mtu anapata ulinzi na manufaa sawa kutoka kwa sheria.
Art. 27(1)
(1) Kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na kupata manufaa sawa ya sheria.
Soma kifungu kamili → - Wanawake na wanaume wana haki sawa na nafasi sawa.
Art. 27(3)
(3) Wanawake na wanaume wana haki ya usawa ikiwemo haki ya kupata nafasi sawa katika shughuli za kisiasa, kiuchumi, kitamaduni na kijamii.
Soma kifungu kamili → - Serikali haipaswi kukubagua kwa sababu yoyote, ikiwemo rangi, jinsia, ujauzito, hali ya ndoa, afya, kabila, rangi ya ngozi, umri, ulemavu, dini, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
Art. 27(4)
(4) Serikali, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, haitakuwa na ubaguzi dhidi ya mtu yeyote kwa misingi yoyote ikiwemo asili, jinsia, ujauzito, hali ya mtu kindoa, hali ya kiafya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
Soma kifungu kamili → - Hakuna mtu anayeruhusiwa kumbagua mtu mwingine.
Art. 27(5)
(5) Mtu hatakuwa na ubaguzi dhidi ya mwingine kwa njia ya moja kwa moja au vinginevyo katika misingi iliyotajwa na kuonyeshwa na ibara ya (4).
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Kila mtu ni sawa mbele ya sheria. Wavulana na wasichana, wakubwa na wadogo, wote wana haki sawa.
Art. 27(1)
(1) Kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na kupata manufaa sawa ya sheria.
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayepaswa kutendewa vibaya kwa sababu ya sura yake, anapotoka, au anachoamini.
Art. 27(4)
(4) Serikali, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, haitakuwa na ubaguzi dhidi ya mtu yeyote kwa misingi yoyote ikiwemo asili, jinsia, ujauzito, hali ya mtu kindoa, hali ya kiafya, asili ya kikabila au kijamii, rangi, umri, ulemavu, dini, dhamiri, imani, utamaduni, mavazi, lugha au kuzaliwa.
Soma kifungu kamili →