Sura 4, Sehemu 2 · Art. 32
Uhuru wa dhamiri, dini, imani na maoni
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni. (2) Kila mtu ana haki, ama kibinafsi au na wengine katika jamii, kwa wazi au kifaragha, kufuata dini au imani yoyote kupitia ibada, matendo, mafundisho au maadhimisho, yakiwemo mazingatio ya siku za ibada. (3) Mtu hatazuiwa kuingia ama kujiunga na taasisi yoyote, kunyimwa ajira au kufika mahali fulani au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani yake ya kidini. (4) Mtu hatalazimishwa kutenda au kujihusisha na kitendo chochote ambacho ni kinyume na imani ya dini yake.
Kwa maneno rahisi
- Kila mtu ana haki ya uhuru wa dhamiri, dini, mawazo, imani na maoni.
Art. 32(1)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni.
Soma kifungu kamili → - Unaweza kufuata na kufundisha dini yako, peke yako au pamoja na wengine, hadharani au faraghani.
Art. 32(2)
(2) Kila mtu ana haki, ama kibinafsi au na wengine katika jamii, kwa wazi au kifaragha, kufuata dini au imani yoyote kupitia ibada, matendo, mafundisho au maadhimisho, yakiwemo mazingatio ya siku za ibada.
Soma kifungu kamili → - Huwezi kunyimwa kazi, huduma au haki kwa sababu ya dini au imani yako.
Art. 32(3)
(3) Mtu hatazuiwa kuingia ama kujiunga na taasisi yoyote, kunyimwa ajira au kufika mahali fulani au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani yake ya kidini.
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayeweza kulazimishwa kufanya jambo kinyume na dini au imani yake.
Art. 32(4)
(4) Mtu hatalazimishwa kutenda au kujihusisha na kitendo chochote ambacho ni kinyume na imani ya dini yake.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Unaweza kuamini unachoamini, na kufuata dini yako, peke yako au pamoja na wengine.
Art. 32(1)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kuwa na msimamo, dini, mawazo, imani na maoni.
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayeweza kukuzuia kwa sababu ya dini yako.
Art. 32(3)
(3) Mtu hatazuiwa kuingia ama kujiunga na taasisi yoyote, kunyimwa ajira au kufika mahali fulani au kufurahia haki yoyote kwa sababu ya imani yake ya kidini.
Soma kifungu kamili →