Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 2 · Art. 34

Uhuru wa vyombo vya habari

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Uhuru na kujitegemea kwa vyombo vya matangazo, kuchapisha na vingine vya
habari ya aina yoyote unahakikishwa lakini hauhusishi masharti yaliyotajwa katika
Kifungu cha 33 (2) .
(2) Serikali –
  (a) haitadhibiti au kuingilia mtu yeyote anayehusika na utangazaji, uchapishaji au
  usambazaji wa chapisho lolote au usambazaji wa habari kwa kutumia nyenzo yoyote;
  au
  (b) haitamwadhibu mtu yeyote kwa kutoa maoni au mawazo au masuala yaliyomo
  kwenye matangazo, machapisho au usambazaji.
(3) Vyombo vya utangazaji na vyombo vingine vya habari na vya kielektroniki vina
uhuru wa kujiendeleza kwa kuongozwa tu na taratibu za leseni ambazo-
  (a) zimeratibiwa kuhakikisha udhibiti wa mawimbi ya hewa na aina nyingine za
  usambazaji wa mawimbi; na
  (b) haviingiliwi na Serikali, maslahi ya kisiasa au ya kibiashara.
(4) Vyombo vyote vya habari vinavyomilikiwa na Serikali-
  (a) vitakuwa huru kuamua kuhusu habari, tahariri na matangazo yao au
  mawasiliano mengine;
  (b) havitaegemea upande wowote; na
  (c) vitatoa nafasi sawa ya kuwasilisha maoni tofauti tofauti na mawazo
  yanayokinzana.
(5) Bunge litatunga sheria itakayotoa nafasi ya kuanzisha shirika ambalo-
  (a) litakuwa huru dhidi ya udhibiti wa Serikali au kuingiliwa kisiasa;
  (b) litaangazia maslahi ya sekta zote za jamii; na
  (c) litaweka viwango na kudhibiti vyombo vya habari na kutathmini uzingativu wa
  viwango hivyo.
Kwa maneno rahisi
  • Uhuru na ujitegemea wa vyombo vya habari umehakikishwa.
    Art. 34(1)

    (1) Uhuru na kujitegemea kwa vyombo vya matangazo, kuchapisha na vingine vya habari ya aina yoyote unahakikishwa lakini hauhusishi masharti yaliyotajwa katika Kifungu cha 33 (2) .

    Soma kifungu kamili →
  • Serikali haipaswi kuingilia au kuadhibu vyombo vya habari kwa kile kinachochapishwa.
    Art. 34(2)

    (2) Serikali – (a) haitadhibiti au kuingilia mtu yeyote anayehusika na utangazaji, uchapishaji au usambazaji wa chapisho lolote au usambazaji wa habari kwa kutumia nyenzo yoyote; au (b) haitamwadhibu mtu yeyote kwa kutoa maoni au mawazo au masuala yaliyomo kwenye matangazo, machapisho au usambazaji.

    Soma kifungu kamili →
  • Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Serikali lazima visiwe na upendeleo na viwape nafasi sawa maoni mbalimbali.
    Art. 34(4)

    (4) Vyombo vyote vya habari vinavyomilikiwa na Serikali- (a) vitakuwa huru kuamua kuhusu habari, tahariri na matangazo yao au mawasiliano mengine; (b) havitaegemea upande wowote; na (c) vitatoa nafasi sawa ya kuwasilisha maoni tofauti tofauti na mawazo yanayokinzana.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Wanahabari wako huru kusema ukweli, na Serikali haipaswi kuwazuia.
    Art. 34(1)

    (1) Uhuru na kujitegemea kwa vyombo vya matangazo, kuchapisha na vingine vya habari ya aina yoyote unahakikishwa lakini hauhusishi masharti yaliyotajwa katika Kifungu cha 33 (2) .

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →