Sura 4, Sehemu 2 · Art. 36
Uhuru wa kutangamana
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana ambayo inahusu haki ya kuanzisha, kujiunga na ,au kushiriki katika majukumu ya mashirika. (2) Mtu hatalazimishwa kujiunga na muungano wa aina yoyote. (3) Sheria yoyote kuhusu usajili wa miungano ya makundi ya kijamii itahitaji kwamba- (a) usajili huo hauwezi kuzuiwa au kuondolewa bila sababu maalum; na (b) kutakuwa na haki ya kusikizwa kwa kesi hiyo kabla ya usajili huo kuvunjiliwa mbali.
Kwa maneno rahisi
- Kila mtu ana haki ya kuanzisha, kujiunga au kushiriki katika chama cha aina yoyote.
Art. 36(1)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana ambayo inahusu haki ya kuanzisha, kujiunga na ,au kushiriki katika majukumu ya mashirika.
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayeweza kulazimishwa kujiunga na chama.
Art. 36(2)
(2) Mtu hatalazimishwa kujiunga na muungano wa aina yoyote.
Soma kifungu kamili → - Kama chama kinatakiwa kusajiliwa, usajili hauwezi kukataliwa au kuondolewa bila sababu.
Art. 36(3)(a)
(a) usajili huo hauwezi kuzuiwa au kuondolewa bila sababu maalum; na
Soma kifungu kamili → - Una haki ya kusikilizwa kwa haki kabla usajili ufutwe.
Art. 36(3)(b)
(b) kutakuwa na haki ya kusikizwa kwa kesi hiyo kabla ya usajili huo kuvunjiliwa mbali.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Unaweza kujiunga na vikundi pamoja na wengine, na hakuna anayeweza kulazimisha ujiunge.
Art. 36(1)
(1) Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana ambayo inahusu haki ya kuanzisha, kujiunga na ,au kushiriki katika majukumu ya mashirika.
Soma kifungu kamili →