Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 2 · Art. 38

Haki za kisiasa

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kila mwananchi ana uhuru wa kuwa na uchaguzi wa kisiasa, ikiwemo haki ya –
  (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa;
  (b) kushiriki katika shughuli za, au kusajili wanachama kwa niaba ya chama cha
  kisiasa; au
  (c) kufanyia kampeni chama cha kisiasa.
(2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika
mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya
mpiga kura kwa -
  (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya
  uchaguzi; na
  (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni
  mwanachama.
(3) Kila raia akiwa mtu mzima ana haki pasipo na masharti yasiyo na busara,-
  (a) kujiandikisha kama mpiga kura;
  (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na
  (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa
  ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.
Kwa maneno rahisi
  • Uko huru kujiunga au kuanzisha chama cha siasa.
    Art. 38(1)(a)

    (a) kuunda, au kushiriki katika uundaji wa chama cha kisiasa;

    Soma kifungu kamili →
  • Kila raia ana haki ya uchaguzi huru na wa haki.
    Art. 38(2)

    (2) Kila mwananchi ana haki ya kushiriki katika uchaguzi huru, wa haki na unaofanyika mara kwa mara kwa misingi ya haki ya kupiga kura kwa wote na uhuru wa hiari ya mpiga kura kwa - (a) shirika au afisi yoyote ya umma iliyobuniwa chini ya Katiba hii na inayofanya uchaguzi; na (b) kiongozi wa afisi yoyote ya chama cha kisiasa ambacho mwananchi huyo ni mwanachama.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama raia mtu mzima, unaweza kujiandikisha kupiga kura.
    Art. 38(3)(a)

    (a) kujiandikisha kama mpiga kura;

    Soma kifungu kamili →
  • Kura yako ni ya siri.
    Art. 38(3)(b)

    (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na

    Soma kifungu kamili →
  • Unaweza kuwa mgombea wa wadhifa wa umma kama unakidhi masharti.
    Art. 38(3)(c)

    (c) kugombea wadhifa katika afisi ya umma, au afisi katika chama cha kisiasa ambacho yeye ni mwanachama na endapo atachaguliwa, ashike usukani.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Ukiwa mkubwa, unaweza kuchagua anayeongoza, na kura yako ni ya siri.
    Art. 38(3)(b)

    (b) kupiga kura ya siri katika uchaguzi wowote au katika kura ya maamuzi; na

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →