Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 2 · Art. 40

Ulinzi wa haki ya kumiliki mali

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kwa kuzingatia Kifungu cha 65, kila mtu ana haki, kibinafsi au kwa kuungana na
wengine kupata na kumiliki mali-
  (a) ya aina yoyote; na
  (b) katika sehemu yoyote ya Kenya.
(2) Bunge halitatunga sheria inayoruhusu Serikali au mtu yeyote –
  (a) kidhalimu kumpokonya mtu mali ya aina yoyote, au thamana ama haki juu ya,
  mali ya aina yoyote;
  (b) kumzuia, au kwa njia yoyote kumnyima kufurahia haki chini ya Kifungu hiki
  katika misingi iliyobainishwa katika Kifungu cha (27) (4).
(3) Serikali haitamnyima mtu yeyote haki ya kuwa na mali ya aina yoyote, au nia au
haki ya kuwa na mali ya aina yoyote isipokuwa endapo kuzuiwa huko-
  (a) kunatokana na upataji ardhi au nia ya kutaka ardhi au kubadilisha maslahi fulani
  ili kupata ardhi, au hatimiliki ya ardhi, kwa mujibu wa Sura ya Tano; au
  (b) ni kwa matumizi ya umma au ni kwa manufaa ya umma na inatekelezwa kwa
  mujibu wa Katiba hii au Sheria nyingine yoyote ya Bunge
  Kwamba-
  (i) inahakikisha malipo kwa ukamilifu ya kumfidia mtu huyo kabla ya mali
  hiyo kuchukuliwa;
  (ii) inampa mtu yeyote, mwenye maslahi au haki juu ya mali hiyo, njia ya
  kufikia mahakama ya kisheria.
(4) Sharti linaweza kuundwa ili kuruhusu fidia kulipwa kwa wakazi wa ardhi kwa nia
nzuri chini ya ibara ya (3), ambao huenda hawana hatimiliki ya ardhi hiyo.
(5) Serikali itaunga mkono, kukuza na kulinda hakimiliki ya usomi kwa watu wa Kenya.
(6) Haki chini ya Kifungu hiki haijumlishi mali yoyote ambayo haijapatikana kisheria.
Kwa maneno rahisi
  • Unaweza kumiliki mali mahali popote nchini Kenya.
    Art. 40(1)

    (1) Kwa kuzingatia Kifungu cha 65, kila mtu ana haki, kibinafsi au kwa kuungana na wengine kupata na kumiliki mali- (a) ya aina yoyote; na (b) katika sehemu yoyote ya Kenya.

    Soma kifungu kamili →
  • Serikali haiwezi kuchukua mali yako isipokuwa kwa manufaa ya umma na ulipwe fidia ya haki mara moja.
    Art. 40(3)(b)

    (b) ni kwa matumizi ya umma au ni kwa manufaa ya umma na inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria nyingine yoyote ya Bunge Kwamba-

    Soma kifungu kamili →
  • Mali iliyopatikana isivyo halali hailindwi na haki hii.
    Art. 40(6)

    (6) Haki chini ya Kifungu hiki haijumlishi mali yoyote ambayo haijapatikana kisheria.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Unaweza kumiliki vitu. Hakuna anayepaswa kuchukua vitu vyako bila sababu nzuri na bila kukulipa.
    Art. 40(3)(b)

    (b) ni kwa matumizi ya umma au ni kwa manufaa ya umma na inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba hii au Sheria nyingine yoyote ya Bunge Kwamba-

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →