Sura 4, Sehemu 2 · Art. 49
Haki za waliotiwa mbaroni
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kila mtu aliyetiwa mbaroni ana haki ya- (a) kuarifiwa kwa upole na kwa lugha anayoielewa, kuhusu- (i) sababu ya kukamatwa; (ii) haki ya kunyamaza; na (iii) matokeo ya kutonyamaza; (b) kunyamaza; (c) kuwasiliana na wakili na watu wengine ambao msaada wao unahitajika; (d) kutolazimishwa kutubu au kukiri hatia, hali ambayo inaweza kutumiwa katika ushahidi dhidi yake; (e) kutenganishwa na watu wanaohudumia vifungo; (f) kufikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo, lakini si baada ya- (i) saa ishirini na nne baada ya kukamatwa; au (ii) iwapo hizo saa ishirini na nne zimekamilika wakati ambapo vikao vya mahakama haviendelei au kwa siku isiyo ya mahakama, kufikia mwisho wa siku ya mahakama inayofuatia; (g) kufunguliwa mashtaka au kuarifiwa kuhusu sababu ya kuendelea kuzuiliwa kwake, au kuachiliwa huru siku yake ya kwanza ya kufikishwa mahakamani; na (h) kuachiliwa kwa dhamana kwa sababu zinazoeleweka kabla ya kushtakiwa isipokuwa kukiwa na sababu nyingine za kulazimisha kutendwa kinyume cha dhamana hiyo. (2) Mtu hatawekwa rumande kwa kosa linaloweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini pekee au kufungwa gerezani kwa muda usiozidi miezi sita.
Kwa maneno rahisi
- Kama umekamatwa, polisi wanapaswa kukuambia sababu, kwa lugha unayoielewa.
Art. 49(1)(a)
(a) kuarifiwa kwa upole na kwa lugha anayoielewa, kuhusu-
Soma kifungu kamili → - Una haki ya kukaa kimya. Huna lazima ya kujieleza.
Art. 49(1)(b)
(b) kunyamaza;
Soma kifungu kamili → - Una haki ya kumpigia wakili, na kuzungumza na watu wanaoweza kukusaidia.
Art. 49(1)(c)
(c) kuwasiliana na wakili na watu wengine ambao msaada wao unahitajika;
Soma kifungu kamili → - Hulazimishwi kukiri au kukubali jambo lolote.
Art. 49(1)(d)
(d) kutolazimishwa kutubu au kukiri hatia, hali ambayo inaweza kutumiwa katika ushahidi dhidi yake;
Soma kifungu kamili → - Lazima upelekwe mahakamani ndani ya saa 24.
Art. 49(1)(f)
(f) kufikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo, lakini si baada ya-
Soma kifungu kamili → - Unaweza kuomba kuachiliwa kwa dhamana isipokuwa kuna sababu kubwa ya kutokuachiliwa.
Art. 49(1)(h)
(h) kuachiliwa kwa dhamana kwa sababu zinazoeleweka kabla ya kushtakiwa isipokuwa kukiwa na sababu nyingine za kulazimisha kutendwa kinyume cha dhamana hiyo.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Kama afisa polisi anakuzuia, lazima akuambie kwa nini, kwa namna unayoelewa.
Art. 49(1)(a)
(a) kuarifiwa kwa upole na kwa lugha anayoielewa, kuhusu-
Soma kifungu kamili → - Unaweza kukaa kimya. Huna lazima ya kujibu.
Art. 49(1)(b)
(b) kunyamaza;
Soma kifungu kamili → - Unaweza kuomba kuzungumza na mtu mzima anayekusaidia, kama wakili au mzazi.
Art. 49(1)(c)
(c) kuwasiliana na wakili na watu wengine ambao msaada wao unahitajika;
Soma kifungu kamili → - Hakuna anayeruhusiwa kukulazimisha kusema ulifanya kosa.
Art. 49(1)(d)
(d) kutolazimishwa kutubu au kukiri hatia, hali ambayo inaweza kutumiwa katika ushahidi dhidi yake;
Soma kifungu kamili → - Unapaswa kupelekwa kwa hakimu haraka sana, ndani ya siku moja.
Art. 49(1)(f)
(f) kufikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo, lakini si baada ya-
Soma kifungu kamili →