Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 2 · Art. 50

Haki katika kusikizwa kwa kesi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kila mtu ana haki ya kutaka mzozo wowote unaoweza kusuluhishwa kisheria
kuamuliwa katika kikao cha haki mahakamani au, ikiwezekana asasi au mahakama
maalum iliyo huru na isiyoegemea upande wowote.
(2) Kila mshtakiwa ana haki ya kesi yake kusikizwa kwa njia ya haki, ikiwemo haki ya-
  (a) kuaminiwa kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe kinyume;
  (b) kuarifiwa kuhusu mashtaka na kupewa taarifa ya kutosha kuyahusu;
  (c) kuwa na wakati na vifaa vya kutosha kutayarisha nyenzo za kujitetea;
  (d) kushtakiwa kwenye mahakama ya umma iliyobuniwa kwa mujibu wa Katiba hii;
  (e) kuanzishwa na kumalizika kwa mashtaka bila kucheleweshwa;
  (f) kuwepo wakati wa kesi isipokuwa pale ambapo mienendo ya mshtakiwa
  inatatiza vikao vya kesi hiyo;
  (g) kuchagua na kuwakilishwa na wakili na kuelezwa kuhusu haki hii moja kwa
  moja;
  (h) kuwa na wakili aliyetolewa na Serikali kwa gharama ya Serikali yenyewe,
  endapo haki yake ya msingi imevunjwa, na aarifiwe kuhusu haki hii moja kwa moja;
  (i) kunyamaza, na kutotoa ushahidi wakati wa kesi;
  (j) kuelezwa mwanzoni kuhusu ushahidi ambao kiongozi wa mashtaka ananuia
  kutumia na kuweza kuufikia ushahidi huo.
  (k) kuleta na kupinga ushahidi;
  (l) kutolazimishwa kutoa ushahidi wa kujifunga;
  (m) kuwa na usaidizi wa mkalimani bila ya kulipishwa endapo mshtakiwa hawezi
  kuelewa lugha inayotumiwa katika kesi;
  (n) kutohukumiwa kwa kitendo, au kosa ambalo wakati wa utendekaji au ukosaji
  halikuwa-
  (i) kosa nchini Kenya; au
  (ii) kosa la jinai chini ya sheria ya kimataifa;
  (o) kutoshtakiwa kwa kosa la kulinganishwa na tendo au kosa ambalo mtu huyo
  amewahi ama kuachiliwa au kuhukumiwa kwalo;
  (p) kunufaika kwa angalau adhabu ndogo kabisa katika adhabu zilizoruhusiwa
  endapo adhabu iliyoidhinishwa kwa kosa lake imebadilishwa kati ya muda wa
  utendekaji wa kosa hilo na wakati wa kuhukumiwa; na
  (q) kukata rufani au kuchunguzwa upya kwa kesi hiyo na mahakama ya ngazi ya juu.
(3) Kila kifungu hiki kinapohitaji taarifa kutolewa kwa mtu, taarifa hiyo itatolewa katika
lugha anayoielewa mtu huyo.
(4) Ushahidi unaopatikana katika njia inayokiuka haki yoyote au uhuru wowote wa
kimsingi uliotolewa katika Sheria ya Haki utaachwa endapo utekelezaji wa ushahidi
huo utafanya kesi kukosa haki au uwe kikwazo katika upatikanaji wa haki.
(5) Mshtakiwa-
  (a) anayeshtakiwa kwa kosa fulani, kando na kosa ambalo mahakama inaweza
  kukamilisha kwa haraka, atakuwa na ruhusa endapo ataomba, ya kupata nakala ya
  rekodi za kesi.
  (b) ana haki ya kupata nakala ya rekodi ya kesi ya vikao vya mashtaka kwa
  wakati unaofaa baada ya kukamilishwa kwa kesi hiyo, kwa malipo fulani kama
  inavyoidhinishwa na sheria.
(6) Mtu aliyehukumiwa kwa kosa la jinai anaweza kulalamikia mahakama kuu ili
kusikizwa upya kwa kesi iwapo-
  (a) rufani yake imetupiliwa mbali na mahakama ya ngazi za juu ambayo mtu huyo
  alikuwa na haki ya kukata rufani, au awe hakukata rufani katika muda unaoruhusiwa
  kufanya hivyo; na
  (b) ushahidi mpya na wa kushawishi umepatikana.
(7) Ili kutimiza haki, mahakama inaweza kuruhusu msuluhishi kusaidia mlalamishi au
mshtakiwa kuwasiliana na mahakama.
(8) Kifungu hiki hakikatazi kuzuiwa kwa vyombo vya habari ama umma kutokuwa
mahakamani, kama kuzuiwa huko ni muhimu, katika jamii huru na ya kidemokrasia,
ili kuwalinda mashahidi, wanyonge, maadili, utulivu wa umma, ama usalama wa
kitaifa.
(9 Bunge litatunga sheria ya kutoa ulinzi, haki na hali ya waathiriwa wa hatia.
Kwa maneno rahisi
  • Kila mgogoro unapaswa kuamuliwa kwa haki na uwazi na mahakama au chombo kisicho na upendeleo.
    Art. 50(1)

    (1) Kila mtu ana haki ya kutaka mzozo wowote unaoweza kusuluhishwa kisheria kuamuliwa katika kikao cha haki mahakamani au, ikiwezekana asasi au mahakama maalum iliyo huru na isiyoegemea upande wowote.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama unashutumiwa kwa kosa, wewe ni mwerevu hadi uthibitishwe kuwa na hatia.
    Art. 50(2)(a)

    (a) kuaminiwa kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe kinyume;

    Soma kifungu kamili →
  • Lazima uambiwe wazi unashutumiwa kwa nini.
    Art. 50(2)(b)

    (b) kuarifiwa kuhusu mashtaka na kupewa taarifa ya kutosha kuyahusu;

    Soma kifungu kamili →
  • Una haki ya wakili, na kuambiwa hivyo mara moja.
    Art. 50(2)(g)

    (g) kuchagua na kuwakilishwa na wakili na kuelezwa kuhusu haki hii moja kwa moja;

    Soma kifungu kamili →
  • Kama kutakuwa na dhuluma kubwa, Serikali inaweza kukupa wakili kwa gharama yake.
    Art. 50(2)(h)

    (h) kuwa na wakili aliyetolewa na Serikali kwa gharama ya Serikali yenyewe, endapo haki yake ya msingi imevunjwa, na aarifiwe kuhusu haki hii moja kwa moja;

    Soma kifungu kamili →
  • Unaweza kukaa kimya na huna lazima ya kutoa ushahidi.
    Art. 50(2)(i)

    (i) kunyamaza, na kutotoa ushahidi wakati wa kesi;

    Soma kifungu kamili →
  • Una haki ya mkalimani bila malipo kama huelewi lugha inayotumika mahakamani.
    Art. 50(2)(m)

    (m) kuwa na usaidizi wa mkalimani bila ya kulipishwa endapo mshtakiwa hawezi kuelewa lugha inayotumiwa katika kesi;

    Soma kifungu kamili →
  • Huwezi kuhukumiwa mara mbili kwa kosa lile lile.
    Art. 50(2)(o)

    (o) kutoshtakiwa kwa kosa la kulinganishwa na tendo au kosa ambalo mtu huyo amewahi ama kuachiliwa au kuhukumiwa kwalo;

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama mtu anasema ulifanya kosa, bado huna hatia hadi ithibitishwe.
    Art. 50(2)(a)

    (a) kuaminiwa kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe kinyume;

    Soma kifungu kamili →
  • Unaweza kuwa na mtu wa kukusaidia kueleza upande wako.
    Art. 50(2)(g)

    (g) kuchagua na kuwakilishwa na wakili na kuelezwa kuhusu haki hii moja kwa moja;

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →