Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 4, Sehemu 3 · Art. 54

Watu Wenye Ulemavu

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Watu wenye ulemavu wana haki ya-
  (a) kuheshimiwa na kupewa heshima ya binadamu ikiwemo, kushughulikiwa,
  kuzungumziwa na kutajwa, kwa njia isiyowadunisha au kuwadhalilisha;
  (b) kupata elimu katika taasisi za elimu na vifaa vya watu wenye ulemavu
  vilivyofungamanishwa na jamii kwa minajili ya maslahi yao;
  (c) kufikia ipasavyo sehemu zote zinazofikwa na umma, usafiri wa umma na habari
  na mawasiliano;
  (d) kutumia lugha ya ishara, Breli, na njia nyingine mwafaka za mawasiliano; na
  (e) kupata nyenzo na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kukabiliana na matatizo ya
  ulemavu huo;
(2) Serikali itahakikisha kuendelea kwa utekelezaji wa kanuni kwamba, angalau asilimia
tano ya maafisa katika mashirika, wanaochaguliwa au kuteuliwa, ni watu wenye
ulemavu.
Kwa maneno rahisi
  • Mtu mwenye ulemavu anapaswa kutendewa kwa heshima na kuzungumziwa kwa namna isiyodhalilisha.
    Art. 54(1)(a)

    (a) kuheshimiwa na kupewa heshima ya binadamu ikiwemo, kushughulikiwa, kuzungumziwa na kutajwa, kwa njia isiyowadunisha au kuwadhalilisha;

    Soma kifungu kamili →
  • Watu wenye ulemavu wana haki ya elimu na huduma zinazowajumuisha katika jamii.
    Art. 54(1)(b)

    (b) kupata elimu katika taasisi za elimu na vifaa vya watu wenye ulemavu vilivyofungamanishwa na jamii kwa minajili ya maslahi yao;

    Soma kifungu kamili →
  • Watu wenye ulemavu wana haki ya kufikia maeneo, usafiri wa umma na taarifa.
    Art. 54(1)(c)

    (c) kufikia ipasavyo sehemu zote zinazofikwa na umma, usafiri wa umma na habari na mawasiliano;

    Soma kifungu kamili →
  • Watu wenye ulemavu wanaweza kutumia lugha ya ishara, Braille au njia nyingine za mawasiliano.
    Art. 54(1)(d)

    (d) kutumia lugha ya ishara, Breli, na njia nyingine mwafaka za mawasiliano; na

    Soma kifungu kamili →
  • Watu wenye ulemavu wanaweza kupata vifaa na zana za kusaidia kuondoa vizuizi.
    Art. 54(1)(e)

    (e) kupata nyenzo na vifaa vinavyoweza kuwasaidia kukabiliana na matatizo ya ulemavu huo;

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Watoto wenye ulemavu wanaweza kwenda shule na kushiriki katika kila kitu.
    Art. 54(1)(b)

    (b) kupata elimu katika taasisi za elimu na vifaa vya watu wenye ulemavu vilivyofungamanishwa na jamii kwa minajili ya maslahi yao;

    Soma kifungu kamili →
  • Kila mtu anapaswa kuweza kutembea na kutumia maeneo kwa urahisi.
    Art. 54(1)(c)

    (c) kufikia ipasavyo sehemu zote zinazofikwa na umma, usafiri wa umma na habari na mawasiliano;

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →