Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 5, Sehemu 1 · Art. 63

Ardhi ya jamii

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Ardhi ya jamii itatolewa na kumilikiwa na jamii zinazotambuliwa kwa misingi ya
kikabila, kitamaduni au mahitaji ya kijamii yanayofanana .
(2) Ardhi ya umma inahusisha-
  (a) ardhi iliyosajiliwa kwa jina la wawakilishi wa kikundi kilicho chini ya masharti
  ya sheria yoyote;
  (b) ardhi yoyote iliyokabidhiwa jamii fulani kupitia kwa njia yoyote ya kisheria;
  (c) ardhi nyingine yoyote itakayotangazwa na Sheria ya Bunge kama ardhi ya jamii;
  na
  (d) ardhi ambayo-
  (e) inamilikiwa kihalali , kusimamiwa au kutumiwa na jamii maalum kama misitu ya
  jamii, malisho ya mifugo au madhabahu;
  (f) ardhi ya kinasaba na ardhi ambayo kitamaduni ilimilikiwa na jamii ya wawindaji;
  au
  (g) kisheria inashikiliwa kama ardhi ya amana na serikali za Kaunti lakini
  isiyojumuisha ardhi ya umma iliyoshikiliwa kama amana na serikali za kaunti chini
  ya Kifungu cha 62 (2).
(3) Ardhi yoyote ya jamii ambayo haijasajiliwa itashikiliwa kwa amana na Serikali za
kaunti kwa niaba ya jamii hizo.
(4) Ardhi ya jamii haitatolewa au kutumiwa vinginevyo isipokuwa kwa misingi ya
sheria inayofafanua hali na viwango vya haki za kila mwanajamii kibinafsi au
wanajamii wote kwa pamoja.
(5) Bunge litatunga sheria kuidhinisha utekelezwaji wa Kifungu hiki.
Kwa maneno rahisi
  • Ardhi ya jamii inamilikiwa na jamii zinazotambulika kwa ukabila, utamaduni au maslahi yanayofanana.
    Art. 63(1)

    (1) Ardhi ya jamii itatolewa na kumilikiwa na jamii zinazotambuliwa kwa misingi ya kikabila, kitamaduni au mahitaji ya kijamii yanayofanana .

    Soma kifungu kamili →
  • Ardhi ya jamii inajumuisha ardhi ya mababu na ardhi inayotumika kama misitu ya jamii, maeneo ya malisho au mahali patakatifu.
    Art. 63(2)(d)

    (d) ardhi ambayo-

    Soma kifungu kamili →
  • Ardhi ya jamii haiwezi kuuzwa au kutumiwa isipokuwa kama sheria inaruhusu.
    Art. 63(4)

    (4) Ardhi ya jamii haitatolewa au kutumiwa vinginevyo isipokuwa kwa misingi ya sheria inayofafanua hali na viwango vya haki za kila mwanajamii kibinafsi au wanajamii wote kwa pamoja.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Ardhi zingine ni za jamii nzima, kama maeneo yao ya malisho, misitu na mahali patakatifu.
    Art. 63(2)(d)

    (d) ardhi ambayo-

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →