Sura 5, Sehemu 1 · Art. 65
Umilikaji Ardhi wa Wasio Raia
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mtu asiye raia anaweza kumiliki au kutumia ardhi kwa misingi ya kukodisha pekee, na mkataba huo hata ukitolewa hautazidi miaka tisini na tisa. (2) Masikizano, makubaliano au uhawilisho wa aina yoyote unaompa mtu asiye raia wa Kenya uwezo wa kumiliki ardhi kwa zaidi ya miaka tisini na tisa utachukuliwa kwamba maafikiano hayo ni ya miaka tisini na tisa na wala sio zaidi. (3) Kwa madhumuni ya Kifungu hiki- (4) kampuni au shirika lolote litakubaliwa tu kama raia iwapo shirika hilo linamilikiwa kabisa na raia mmoja au zaidi; (5) mali inayoshikiliwa kama amana itachukuliwa kama inayomilikiwa na raia iwapo tu faida ya manufaa yote ya amana hiyo inashikiliwa na raia. (6) Bunge linaweza kutunga sheria kuweka masharti zaidi ya utekelezaji wa Kifungu hiki.
Kwa maneno rahisi
- Mtu ambaye si raia anaweza kumiliki ardhi kwa kukodisha tu, kwa muda usiozidi miaka 99.
Art. 65(1)
(1) Mtu asiye raia anaweza kumiliki au kutumia ardhi kwa misingi ya kukodisha pekee, na mkataba huo hata ukitolewa hautazidi miaka tisini na tisa.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Watu ambao si raia wa Kenya wanaweza kukodisha ardhi tu, sio kumiliki milele.
Art. 65(1)
(1) Mtu asiye raia anaweza kumiliki au kutumia ardhi kwa misingi ya kukodisha pekee, na mkataba huo hata ukitolewa hautazidi miaka tisini na tisa.
Soma kifungu kamili →