Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 5, Sehemu 1 · Art. 67

Tume ya Kitaifa ya Ardhi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Tume ya Kitaifa ya Ardhi imeundwa.
(2) Majukumu ya Tume ya Kitaifa ya Ardhi ni-
  (a) kusimamia ardhi ya umma kwa niaba ya Serikali ya kitaifa na kaunti;
  (b) kupendekezea Serikali ya kitaifa sera ya kitaifa kuhusu ardhi;
  (c) kushauri Serikali ya kitaifa kuhusu utaratibu wa kina wa kusajili umiliki wa
  ardhi kote nchini.
  (d) kufanya utafiti kuhusiana na ardhi na matumizi ya rasilmali nyingine za kiasili
  na kutoa mapendekezo kwa mamlaka yanayohusika;
  (e) kuanzisha uchunguzi wake au kutokana na malalamiko kuhusu ukiuakaji haki
  uliopo au wa kihistoria kuhusu ardhi na kupendekeza suluhisho mwafaka;
  (f) kuhimiza matumizi ya njia za kiasili zinazokubalika za kusuluhisha mizozo
  inayohusu ardhi;
  (g) kutathmini ushuru unaotozwa ardhi na thamani ya mali isiyoweza kuhamishwa
  katika eneo lolote linalotambuliwa na sheria;
  (h) kusimamia na kuwa na jukumu la kuangalia mpango wa matumizi ya ardhi
  nchini;
(3) Tume ya Kitaifa ya Ardhi inaweza kutekeleza majukumu mengine yatakayotolewa
na sheria ya nchi.
Kwa maneno rahisi
  • Kenya ina Tume ya Kitaifa ya Ardhi.
    Art. 67(1)

    (1) Tume ya Kitaifa ya Ardhi imeundwa.

    Soma kifungu kamili →
  • Tume inasimamia ardhi ya umma kwa niaba ya serikali ya kitaifa na za kaunti.
    Art. 67(2)(a)

    (a) kusimamia ardhi ya umma kwa niaba ya Serikali ya kitaifa na kaunti;

    Soma kifungu kamili →
  • Inachunguza dhuluma za ardhi za sasa au za kihistoria na kupendekeza ufumbuzi.
    Art. 67(2)(e)

    (e) kuanzisha uchunguzi wake au kutokana na malalamiko kuhusu ukiuakaji haki uliopo au wa kihistoria kuhusu ardhi na kupendekeza suluhisho mwafaka;

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kuna ofisi maalum inayotunza ardhi ya umma na kusikiliza malalamiko ya ardhi.
    Art. 67(2)(a)

    (a) kusimamia ardhi ya umma kwa niaba ya Serikali ya kitaifa na kaunti;

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →