Sura 6 · Art. 73
Majukumu ya uongozi
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mamlaka yaliyotolewa kwa afisa wa Serikali- (a) ni amana ya umma inayopaswa kutekelezwa katika njia ambayo- (i) inaambatana na majukumu na makusudi ya Katiba hii; (ii) inadhihirisha heshima kwa watu; (iii) inaleta sifa katika taifa na hadhi kwenye afisi; na (iv) inakuza imani ya umma katika maadili ya kiafisi; na (b) yanampa afisa huyo wa Serikali jukumu la kuhudumia watu badala ya nguvu za kuwatawala. (2) Kanuni zinazotoa mwongozo wa uongozi na maadili ni – (a) uteuzi kwa misingi ya uadilifu, ustadi wa kufanya kazi, kufaa kwake, au uchaguzi huru na wa haki; (b) kutopendelea katika maamuzi na katika kuhakikisha kwamba maamuzi hayo hayatokani na mapendeleo ya kindugu au nia zingine zozote mbaya au vitendo vya ufisadi; (c) huduma za kujitolea kwa misingi hasa ya manufaa ya umma, ikidhihirishwa na – (i) uaminifu katika utekelezaji wa wajibu kwa umma; na; (ii) kutangaza maslahi ya kibinafsi yanayoweza kugongana na wajibu wake kwa umma; (d) uwajibikaji kwa umma kuhusu maamuzi na hatua zinazochukuliwa; na (e) nidhamu na kujitolea katika kuhudumia watu.
Kwa maneno rahisi
- Mamlaka anayopewa afisa wa Serikali ni uaminifu wa umma, kutekelezwa kwa heshima kwa wananchi na kuleta heshima kwa ofisi.
Art. 73(1)(a)
(a) ni amana ya umma inayopaswa kutekelezwa katika njia ambayo-
Soma kifungu kamili → - Jukumu la afisa wa Serikali ni kuwatumikia wananchi, sio kuwatawala.
Art. 73(1)(b)
(b) yanampa afisa huyo wa Serikali jukumu la kuhudumia watu badala ya nguvu za kuwatawala.
Soma kifungu kamili → - Kanuni za uongozi ni pamoja na kutokuwa na upendeleo, uaminifu, kutangaza maslahi binafsi, na uwajibikaji.
Art. 73(2)
(2) Kanuni zinazotoa mwongozo wa uongozi na maadili ni – (a) uteuzi kwa misingi ya uadilifu, ustadi wa kufanya kazi, kufaa kwake, au uchaguzi huru na wa haki; (b) kutopendelea katika maamuzi na katika kuhakikisha kwamba maamuzi hayo hayatokani na mapendeleo ya kindugu au nia zingine zozote mbaya au vitendo vya ufisadi; (c) huduma za kujitolea kwa misingi hasa ya manufaa ya umma, ikidhihirishwa na – (i) uaminifu katika utekelezaji wa wajibu kwa umma; na; (ii) kutangaza maslahi ya kibinafsi yanayoweza kugongana na wajibu wake kwa umma; (d) uwajibikaji kwa umma kuhusu maamuzi na hatua zinazochukuliwa; na (e) nidhamu na kujitolea katika kuhudumia watu.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Viongozi wapo kuwatumikia watu, sio kuwatawala.
Art. 73(1)(b)
(b) yanampa afisa huyo wa Serikali jukumu la kuhudumia watu badala ya nguvu za kuwatawala.
Soma kifungu kamili →