Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 7, Sehemu 2 · Art. 90

Ugawaji wa orodha ya viti vya chama

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Uchaguzi wa viti bungeni uliotolewa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b),
  (c) na (d), na wanachama wa baraza la kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na
  (c),utakuwa kwa misingi ya ushirikishwaji sawa kwa kutumia orodha za vyama.
(2) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka itawajibika katika kuendesha na kusimamia
chaguzi za viti vilivyotolewa chini ya Ibara ya (1) na itahakikisha kwamba-
  (a) kila chama cha kisiasa kinachoshiriki katika uchaguzi mkuu kitateua na
  kuwasilisha orodha ya majina ya watu wote ambao wangalichaguliwa iwapo
  chama hicho kingalipewa viti vyote kama ilivyo chini ya Ibara ya (1), kwa wakati
  ulioagizwa kupitia sheria ya kitaifa;
  (b) isipokuwa kwenye viti vilivyoelezewa chini ya Kifungu cha cha 98 (1) (b), kila
  orodha ya vyama ina idadi kamilifu ya wagombeaji wanaostahili na hubadilishana
  kati ya wagombeaji wanaume na wanawake kulingana na jinsi walivyoorodheshwa ;
  na
  (c) isipokuwa kwenye viti vya baraza la kaunti, kila orodha ya chama inaakisi tofauti
  za kimaeneo na uanuwai wa kikabila wa Wakenya.
(3) Viti vilivyotajwa katika ibara ya (1) vitagawiwa vyama vya kisiasa kwa kulingana
na idadi ya jumla ya viti walivyoshinda wagombeaji wa chama cha kisiasa katika
uchaguzi mkuu.
Kwa maneno rahisi
  • Viti vingine hujazwa kwa orodha za vyama, kwa misingi ya uwakilishi sawia.
    Art. 90(1)

    (1) Uchaguzi wa viti bungeni uliotolewa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na wanachama wa baraza la kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c),utakuwa kwa misingi ya ushirikishwaji sawa kwa kutumia orodha za vyama.

    Soma kifungu kamili →
  • Orodha za vyama zinabadilishana kati ya wagombea wa kiume na wa kike.
    Art. 90(2)(b)

    (b) isipokuwa kwenye viti vilivyoelezewa chini ya Kifungu cha cha 98 (1) (b), kila orodha ya vyama ina idadi kamilifu ya wagombeaji wanaostahili na hubadilishana kati ya wagombeaji wanaume na wanawake kulingana na jinsi walivyoorodheshwa ; na

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Viti vingine maalum hugawanywa kati ya vyama, na orodha zinabadilishana kati ya wanaume na wanawake.
    Art. 90(1)

    (1) Uchaguzi wa viti bungeni uliotolewa chini ya Kifungu cha 97 (1) (c) na 98 (1) (b), (c) na (d), na wanachama wa baraza la kaunti chini ya kifungu cha 177 (1) (b) na (c),utakuwa kwa misingi ya ushirikishwaji sawa kwa kutumia orodha za vyama.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →