Sura 8, Sehemu 1 · Art. 94
Jukumu la Bunge
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mamlaka ya utungaji wa sheria ya Jamhuri hii inatokana na wananchi na katika kiwango cha kitaifa, yamekabidhiwa kwa na kutekelezwa na Bunge. (2) Bunge hufuatilia uanuwai wa taifa, huwakilisha nia ya wananchi, na hutekeleza Mamlaka yao. (3) Bunge linaweza kukubali na kupitisha marekebisho kwenye Katiba hii na kubadilisha mipaka ya kaunti kama inavyoagizwa katika Katiba hii; (4) Bunge litalinda Katiba hii na kudumisha utawala wa kidemokrasia katika Jamhuri hii. (5) Hakuna mtu yeyote au asasi yoyote, isipokuwa Bunge, itakayokuwa na mamlaka ya kuunda masharti yatakayokuwa na nguvu za kisheria nchini Kenya isipokuwa kwa amri ya Katiba hii iliyokabidhiwa Bunge au kwa Sheria ya Bunge. (6) Sheria ya Bunge, au sheria ya kaunti, inayoipatia asasi yoyote ya Serikali, afisa wa Serikali, au mtu yeyote mamlaka ya kutunga masharti au sheria na kuipatia nguvu za kisheria nchini Kenya, kama inavyokusudiwa katika Ibara ya (5), itaeleza bayana na kwa hakika shabaha na malengo ya kukabidhiwa mamlaka haya, viwango vya mamlaka, hali na upeo wa sheria zitakavyotungwa, na kanuni na viwango vya ubora vinavyotumika kisheria na vilivyobuniwa chini ya mamlaka haya.
Kwa maneno rahisi
- Mamlaka ya kutunga sheria ya Jamhuri yanatoka kwa wananchi na hutekelezwa na Bunge katika ngazi ya kitaifa.
Art. 94(1)
(1) Mamlaka ya utungaji wa sheria ya Jamhuri hii inatokana na wananchi na katika kiwango cha kitaifa, yamekabidhiwa kwa na kutekelezwa na Bunge.
Soma kifungu kamili → - Bunge lazima lilinde Katiba na kukuza utawala wa kidemokrasia.
Art. 94(4)
(4) Bunge litalinda Katiba hii na kudumisha utawala wa kidemokrasia katika Jamhuri hii.
Soma kifungu kamili → - Ni Bunge pekee lenye mamlaka ya kutunga sheria zenye nguvu ya kisheria nchini Kenya, isipokuwa pale Katiba inaruhusu vinginevyo.
Art. 94(5)
(5) Hakuna mtu yeyote au asasi yoyote, isipokuwa Bunge, itakayokuwa na mamlaka ya kuunda masharti yatakayokuwa na nguvu za kisheria nchini Kenya isipokuwa kwa amri ya Katiba hii iliyokabidhiwa Bunge au kwa Sheria ya Bunge.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Bunge hutunga sheria za nchi, na mamlaka yake yanatoka kwa wananchi.
Art. 94(1)
(1) Mamlaka ya utungaji wa sheria ya Jamhuri hii inatokana na wananchi na katika kiwango cha kitaifa, yamekabidhiwa kwa na kutekelezwa na Bunge.
Soma kifungu kamili →