Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 1 · Art. 95

Majukumu ya Baraza la Kitaifa

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Baraza la Kitaifa linawakilisha watu wa maeneobunge na walio na maslahi maalumu
katika Baraza la Kitaifa.
(2) Baraza la Kitaifa hushauriana kuhusu na kusuluhisha masuala yenye umuhimu
mkubwa kwa watu.
(3) Baraza la Kitaifa linatunga sheria kwa kuzingatia Sehemu ya 4 ya Sura hii.
(4) Baraza la Kitaifa -
  (a) hubainisha ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama
  inavyoagizwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili;
  (b) hugawa hazina ya fedha kwa matumizi ya Serikali ya kitaifa na asasi nyingine za
  Serikali ya kitaifa; na
  (c) hutekeleza usimamizi wa jumla wa mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake.
(5) Baraza la Kitaifa-
  (a) linachunguza utendakazi wa Rais afisini, Naibu wa rais na maafisa wengine wa
  Serikali na ikiwezekana kuchukua hatua za kuwatoa afisini; na
  (b) litasimamia asasi za Serikali;
(6) Baraza la Kitaifa litaidhinisha tangazo la vita na kutathmini ongezeko la hali ya
hatari nchini.
Kwa maneno rahisi
  • Bunge la Kitaifa linawakilisha wananchi wa maeneo bunge na maslahi maalum.
    Art. 95(1)

    (1) Baraza la Kitaifa linawakilisha watu wa maeneobunge na walio na maslahi maalumu katika Baraza la Kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
  • Hutunga sheria, hugawa mapato ya kitaifa na husimamia matumizi yake.
    Art. 95(4)

    (4) Baraza la Kitaifa - (a) hubainisha ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama inavyoagizwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili; (b) hugawa hazina ya fedha kwa matumizi ya Serikali ya kitaifa na asasi nyingine za Serikali ya kitaifa; na (c) hutekeleza usimamizi wa jumla wa mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake.

    Soma kifungu kamili →
  • Huidhinisha matangazo ya vita na kuongezwa kwa hali ya dharura.
    Art. 95(6)

    (6) Baraza la Kitaifa litaidhinisha tangazo la vita na kutathmini ongezeko la hali ya hatari nchini.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Bunge la Kitaifa hutunga sheria na kuchunguza jinsi fedha za umma zinatumika.
    Art. 95(4)

    (4) Baraza la Kitaifa - (a) hubainisha ugavi wa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama inavyoagizwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili; (b) hugawa hazina ya fedha kwa matumizi ya Serikali ya kitaifa na asasi nyingine za Serikali ya kitaifa; na (c) hutekeleza usimamizi wa jumla wa mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →