Sura 8, Sehemu 1 · Art. 96
Jukumu la Seneti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Seneti inawakilisha kaunti na inatumika kulinda maslahi ya kaunti na serikali zake; (2) Seneti inashiriki katika jukumu la Bunge la uundaji wa sheria kwa kuamua, kujadiliana, kuidhinisha miswada inayohusu kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 109 hadi 113. (3) Seneti ndio huamua ugavi wa mapato ya kitaifa miongoni mwa kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 217, na kutekeleza usimamizi jumla wa mapato ya kitaifa iliyotengewa kwa serikali za kaunti. (4) Seneti inashiriki katika usimamizi wa maafisa wa Serikali na kutathmini na kutoa maamuzi kuhusu hoja ya kumuondoa Rais au Naibu wa rais kutoka kwenye wadhifa wake kwa mujibu wa Kifungu cha 145.
Kwa maneno rahisi
- Seneti inawakilisha kaunti na kulinda maslahi ya kaunti na serikali zao.
Art. 96(1)
(1) Seneti inawakilisha kaunti na inatumika kulinda maslahi ya kaunti na serikali zake;
Soma kifungu kamili → - Seneti huzingatia, kujadili na kuidhinisha Miswada inayohusu kaunti.
Art. 96(2)
(2) Seneti inashiriki katika jukumu la Bunge la uundaji wa sheria kwa kuamua, kujadiliana, kuidhinisha miswada inayohusu kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 109 hadi 113.
Soma kifungu kamili → - Seneti huamua mgawanyo wa mapato ya kitaifa kati ya kaunti.
Art. 96(3)
(3) Seneti ndio huamua ugavi wa mapato ya kitaifa miongoni mwa kaunti kama ilivyo katika Kifungu cha 217, na kutekeleza usimamizi jumla wa mapato ya kitaifa iliyotengewa kwa serikali za kaunti.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Seneti huzungumzia kaunti na kutunza maslahi yao.
Art. 96(1)
(1) Seneti inawakilisha kaunti na inatumika kulinda maslahi ya kaunti na serikali zake;
Soma kifungu kamili →