Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 2 · Art. 98

Uanachama wa Seneti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Seneti itajumuisha-
  (a) wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na
  wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, na kila kaunti ikiwa ni eneowakilishi la
  mwanachama mmoja;
  (b) wanachama wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa
  kulingana na usawa wao wa wanachama kwenye Seneti waliochaguliwa chini ya
  ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90;
  (c) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ili
  kuwakilisha vijana;
  (d) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja
  wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na
  (e) Spika atakayekuwa mwanachama m’badala kwa mujibu wa wadhifa wake.
(2) Wanachama waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kwa mujibu wa
Kifungu cha 90.
(3) Hakuna chochote katika Kifungu hiki kitafasiriwa kama kinachomuondoa mtu
yeyote katika ugombeaji wa uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).
Kwa maneno rahisi
  • Seneti ina wajumbe 47 waliochaguliwa (mmoja kwa kila kaunti), wanawake 16 walioteuliwa, wajumbe wanaowakilisha vijana na watu wenye ulemavu, na Spika.
    Art. 98(1)

    (1) Seneti itajumuisha- (a) wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa kwenye kaunti, na kila kaunti ikiwa ni eneowakilishi la mwanachama mmoja; (b) wanachama wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na usawa wao wa wanachama kwenye Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kwa mujibu wa Kifungu cha 90; (c) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja ili kuwakilisha vijana; (d) wanachama wawili wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja wakiwakilisha watu wenye ulemavu; na (e) Spika atakayekuwa mwanachama m’badala kwa mujibu wa wadhifa wake.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Seneti ina mjumbe mmoja aliyechaguliwa kwa kila kaunti kati ya 47, pamoja na wengine.

    Tafuta →