Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 2 · Art. 101

Uchaguzi wa Wabunge

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika
kila mwaka wa tano.
(2) panapotokea nafasi katika afisi ya mbunge wa Baraza la Kitaifa, lililotajwa chini ya
Kifungu cha 97 (1) (c), au katika Seneti chini ya Kifungu cha 98 (1) (b), (c) ama
  (d), Spika mhusika, katika kipindi cha siku ishirini na moja za kutokea nafasi hiyo ya
  kazi, atatoa notisi kwa maandishi kuhusu nafasi hiyo ya kazi kwa-
  (a) Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka; na
  (b) chama cha kisiasa ambacho kupitia kwa orodha yake ya chama ndipo
  mwanachama huyo alipokuwa amechaguliwa au kuteuliwa.
(3) Nafasi hiyo iliyotajwa katika Ibara ya (2) kwa, kuambatana na Ibara ya (5), itajazwa
kwa namna iliyoagizwa na Sheria ya Bunge ndani ya muda wa siku ishirini na moja
baada ya kutangazwa na Spika mhusika.
(4) Panapotokea nafasi ya kazi katika afisi ya mwanachama wa Baraza la Kitaifa
aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha 97 (1) (a) au (b), au wa Seneti aliyechaguliwa
chini ya Kifungu cha 98 (1) (a)-
  (a) Spika mhusika, kwa muda wa siku ishirini na moja baada ya kutokea kwa nafasi
  hii, atatoa notisi kuhusu nafasi hii kwa kuiandikia Tume Huru ya Uchaguzi na
  Mipaka; na
  (b) uchaguzi mdogo utafanyika katika muda wa siku tisini baada ya kutokea kwa
  nafasi hiyo ya kazi, kuambatana na ibara ya (5).
(5) Nafasi iliyotajwa katika ibara ya (4) haitajazwa katika kipindi cha miezi mitatu
inayotangulia uchaguzi mkuu.
Kwa maneno rahisi
  • Uchaguzi mkuu wa wabunge hufanyika Jumanne ya pili ya Agosti kila mwaka wa tano.
    Art. 101(1)

    (1) Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika kila mwaka wa tano.

    Soma kifungu kamili →
  • Uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi iliyoachwa lazima ufanyike ndani ya siku 90.
    Art. 101(4)(b)

    (b) uchaguzi mdogo utafanyika katika muda wa siku tisini baada ya kutokea kwa nafasi hiyo ya kazi, kuambatana na ibara ya (5).

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Wabunge huchaguliwa kila baada ya miaka mitano, mwezi Agosti.
    Art. 101(1)

    (1) Uchaguzi mkuu wa wabunge utafanyika Jumanne ya pili ya mwezi wa Agosti katika kila mwaka wa tano.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →