Sura 8, Sehemu 3 · Art. 108
Viongozi wa vyama
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Kutakuwa na Kiongozi wa chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge na kiongozi wa chama cha walio wachache Bungeni. (2) Kiongozi wa chama kilicho na wabunge wengi ndiye atakayekuwa kiongozi katika Baraza la Kitaifa la chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge au muungano wa vyama; (3) Kiongozi wa chama cha walio wachache ni kiongozi katika Baraza la Kitaifa la chama kilicho cha pili kwa idadi ya wabunge au muungano wa vyama; (4) Mpangilio ufuatao wa kupewa umuhimu wa kwanza utafuatwa katika Baraza la Kitaifa – (a) Spika wa Baraza la Kitaifa; (b) Kiogozi wa chama cha wabunge walio wengi; (c) Kiongozi wa chama cha wabunge walio wachache.
Kwa maneno rahisi
- Kuna kiongozi wa chama cha walio wengi na kiongozi wa chama cha walio wachache katika Bunge la Kitaifa.
Art. 108(1)
(1) Kutakuwa na Kiongozi wa chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge na kiongozi wa chama cha walio wachache Bungeni.
Soma kifungu kamili → - Kiongozi wa chama cha walio wengi ni kiongozi wa chama kikubwa zaidi au muungano wa vyama.
Art. 108(2)
(2) Kiongozi wa chama kilicho na wabunge wengi ndiye atakayekuwa kiongozi katika Baraza la Kitaifa la chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge au muungano wa vyama;
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Katika Bunge la Kitaifa, chama kikubwa zaidi kina kiongozi, na cha pili kikubwa pia kina kimoja.
Art. 108(1)
(1) Kutakuwa na Kiongozi wa chama kilicho na idadi kubwa ya wabunge na kiongozi wa chama cha walio wachache Bungeni.
Soma kifungu kamili →