Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 4 · Art. 110

Miswada kuhusu Serikali za Kaunti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Katika Katiba hii, ‘Mswada unaohusu serikali ya kaunti unamaanisha’-
  (a) mswada ulio na masharti yanayoathiri majukumu na mamlaka ya serikali za
  kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Nne; na
  (b) Mswada unaohusiana na uchaguzi wa mwanachama wa bunge la kaunti au
  serikali za kaunti.
  (c ) mswada uliotajwa katika Sura ya Kumi na mbili unaoathiri fedha za serikali za
  kaunti.
(2) Mswada unaohusu serikali za kaunti ni-
  (a) mswada maalumu ambao utashughulikiwa chini ya Kifungu cha 111, iwapo-
  (i) unahusiana na uchaguzi wa wabunge wa bunge la kaunti au serikali ya
  kaunti; au
  (ii) ni Mswada wa Mgao wa Mapato ya Kaunti wa kila mwaka uliotajwa katika
  Kifungu cha 218; au
  (iii) mswada wa kawaida ambao utashughulikiwa chini ya Kifungu cha 112
  katika hali yoyote.
(3) Kabla ya mojawapo ya vitengo vya Bunge kutathmini mswada, Maspika wa Baraza
la Kitaifa na Seneti kwa pamoja wataamua suala lolote kuhusu kama Mswada huo
unahusu kaunti na iwapo ni hivyo, kama ni mswada maalumu au wa kawaida.
(4) Wakati Mswada unahusu serikali za kaunti umepitishwa na Bunge moja, Spika wa
Bunge hilo ataupeleka kwa Spika wa Bunge hilo jingine.
(5) Iwapo Mabunge yote mawili yatapitisha Mswada katika mfumo uleule, Spika wa
Bunge ulikotoka mswada huo, ataupeleka kwa Rais katika muda wa siku saba ili
uidhinishwe.
Kwa maneno rahisi
  • Mswada unaohusu serikali ya kaunti ni ule unaoathiri majukumu au mamlaka ya serikali za kaunti, uchaguzi wa maafisa wa kaunti, au fedha za kaunti.
    Art. 110(1)

    (1) Katika Katiba hii, ‘Mswada unaohusu serikali ya kaunti unamaanisha’- (a) mswada ulio na masharti yanayoathiri majukumu na mamlaka ya serikali za kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Nne; na (b) Mswada unaohusiana na uchaguzi wa mwanachama wa bunge la kaunti au serikali za kaunti. (c ) mswada uliotajwa katika Sura ya Kumi na mbili unaoathiri fedha za serikali za kaunti.

    Soma kifungu kamili →
  • Kabla Baraza lolote kuzingatia Mswada, Spika huamua kwa pamoja kama unahusu kaunti.
    Art. 110(3)

    (3) Kabla ya mojawapo ya vitengo vya Bunge kutathmini mswada, Maspika wa Baraza la Kitaifa na Seneti kwa pamoja wataamua suala lolote kuhusu kama Mswada huo unahusu kaunti na iwapo ni hivyo, kama ni mswada maalumu au wa kawaida.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Miswada mingine huathiri kaunti, na Bunge huamua jinsi ya kuishughulikia.
    Art. 110(1)

    (1) Katika Katiba hii, ‘Mswada unaohusu serikali ya kaunti unamaanisha’- (a) mswada ulio na masharti yanayoathiri majukumu na mamlaka ya serikali za kaunti zilizotajwa katika Mpangilio wa Nne; na (b) Mswada unaohusiana na uchaguzi wa mwanachama wa bunge la kaunti au serikali za kaunti. (c ) mswada uliotajwa katika Sura ya Kumi na mbili unaoathiri fedha za serikali za kaunti.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →