Sura 8, Sehemu 4 · Art. 111
Miswada maalumu inayohusu serikali za kaunti
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mswada maalumu unaohusu serikali za kaunti utashughulikiwa kwa namna moja kama mswada wa kawaida unaohusu serikali za kaunti kuambatana na ibara ya ya (2) na (3). (2) Baraza la Kitaifa linaweza kurekebisha au kupiga marufuku mswada maalum uliopitishwa na Seneti kwa uamuzi tu ulioungwa mkono na angalau thuluthi mbili ya wabunge. (3) Iwapo uamuzi katika Baraza la Kitaifa wa kurekebisha au kupiga marufuku mswada maalum utaangushwa, Spika wa Bunge ataupeleka mswada kwa hali iliyokubaliwa na Seneti kwa Rais katika muda wa siku saba ili kuidhinishwa.
Kwa maneno rahisi
- Bunge la Kitaifa linaweza kurekebisha au kukataa Mswada maalum uliopitishwa na Seneti kwa azimio linaloungwa mkono na angalau theluthi mbili ya wajumbe wake.
Art. 111(2)
(2) Baraza la Kitaifa linaweza kurekebisha au kupiga marufuku mswada maalum uliopitishwa na Seneti kwa uamuzi tu ulioungwa mkono na angalau thuluthi mbili ya wabunge.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Kwa Miswada maalum kuhusu kaunti, mabaraza mawili lazima yakubaliane, na Bunge la Kitaifa linahitaji wingi mkubwa kubadilisha toleo la Seneti.
Art. 111(2)
(2) Baraza la Kitaifa linaweza kurekebisha au kupiga marufuku mswada maalum uliopitishwa na Seneti kwa uamuzi tu ulioungwa mkono na angalau thuluthi mbili ya wabunge.
Soma kifungu kamili →