Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 4 · Art. 113

Kamati za Upatanishi

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Iwapo Mswada utapelekwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 112,
Maspika wa Mabunge yote mawili watateua kamati ya upatanishi itakayohusisha
idadi sawa ya wanachama wa Mabunge yote mawili ili kujaribu kutengeneza toleo
jingine la Mswada litakalokubalika na Mabunge yote mawili.
(2) Iwapo kamati ya upatanishi itakubaliana na toleo hilo la Mswada, basi kila Bunge
litapiga kura ili kupitisha au kukataa toleo hilo la Mswada.
(3) Iwapo Mabunge yote mawili yanakubali ttole hilo la Mswada kama
ilivyopendekezwa na kamati ya upatanishi, Spika wa Baraza la Kitaifa atamkabidhi
Rais ili kuidhinishwa.
(4) Iwapo kamati ya upatanishi itakosa kuafikiana kuhusu toleo hilo la Mswada kwa
kipindi cha muda wa siku thelathini, au iwapo toleo hilo lililopendekezwa na kamati
litakataliwa na na mojawapo ya Mabunge, basi Mswada huo utakuwa umeshindwa.
Kwa maneno rahisi
  • Kama Mswada unapelekwa kwa kamati ya upatanishi, Spika huteua kamati yenye wajumbe sawa kutoka kila Baraza ili kupata toleo ambalo mabaraza yote yatapitisha.
    Art. 113(1)

    (1) Iwapo Mswada utapelekwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 112, Maspika wa Mabunge yote mawili watateua kamati ya upatanishi itakayohusisha idadi sawa ya wanachama wa Mabunge yote mawili ili kujaribu kutengeneza toleo jingine la Mswada litakalokubalika na Mabunge yote mawili.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama kamati ikishindwa kukubaliana ndani ya siku 30, Mswada unashindwa.
    Art. 113(4)

    (4) Iwapo kamati ya upatanishi itakosa kuafikiana kuhusu toleo hilo la Mswada kwa kipindi cha muda wa siku thelathini, au iwapo toleo hilo lililopendekezwa na kamati litakataliwa na na mojawapo ya Mabunge, basi Mswada huo utakuwa umeshindwa.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kikundi maalum cha wajumbe sawa kutoka mabaraza yote kinajaribu kukubaliana; wakishindwa, Mswada unashindwa.
    Art. 113(1)

    (1) Iwapo Mswada utapelekwa kwa kamati ya upatanishi chini ya Kifungu cha 112, Maspika wa Mabunge yote mawili watateua kamati ya upatanishi itakayohusisha idadi sawa ya wanachama wa Mabunge yote mawili ili kujaribu kutengeneza toleo jingine la Mswada litakalokubalika na Mabunge yote mawili.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →