Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 4 · Art. 114

Miswada ya Fedha

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mswada wa fedha hauwezi kushughulikia suala jingine lolote isipokuwa tu lile
ambalo limeorodheshwa katika fasiri ya ‘Mswada wa fedha’ kwenye ibara ya (3).
(2) iwapo, kwa maoni ya Spika wa Baraza la Kitaifa, mjadala unatoa vifungu kwa suala
lililotajwa katika fasiri ya Mswada wa fedha, Bunge linaweza kuendelea tu kwa
mujibu wa mapendekezo ya kamati husika ya Bunge baada ya kutilia maanani maoni
ya Waziri anayehusika na fedha.
(3) Katika Katiba hii, ‘Mswada wa fedha’ unamaanisha, Mswada, tofauti na Mswada
uliotajwa katika Kifungu cha 218 kilicho na masharti yanayoshughulikia-
  (a) ushuru;
  (b) kutoza malipo kwa hazina ya umma au kubadili au kuondolewa kwa mojawapo
  wa malipo hayo;
  (c) kugawa, kupokea, kutunza, kuwekeza au kutoa pesa za umma;
  (d) kudhamini mkopo wowote au ulipwaji wake; ama
  (e) masuala mengineyo yanayotokana na masuala hayo.
(4) Katika ibara ya (3), “ushuru”, “fedha za umma”, na “mkopo”, hazijumuishi ushuru
wowote, fedha za umma au mkopo uliopatwa na kaunti.
Kwa maneno rahisi
  • Mswada wa fedha unahusu tu kodi, gharama kwa fedha za umma, fedha za umma, au mikopo.
    Art. 114(3)

    (3) Katika Katiba hii, ‘Mswada wa fedha’ unamaanisha, Mswada, tofauti na Mswada uliotajwa katika Kifungu cha 218 kilicho na masharti yanayoshughulikia- (a) ushuru; (b) kutoza malipo kwa hazina ya umma au kubadili au kuondolewa kwa mojawapo wa malipo hayo; (c) kugawa, kupokea, kutunza, kuwekeza au kutoa pesa za umma; (d) kudhamini mkopo wowote au ulipwaji wake; ama (e) masuala mengineyo yanayotokana na masuala hayo.

    Soma kifungu kamili →
  • Mswada wa fedha unaweza kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa pekee.
    Art. 114(1)

    (1) Mswada wa fedha hauwezi kushughulikia suala jingine lolote isipokuwa tu lile ambalo limeorodheshwa katika fasiri ya ‘Mswada wa fedha’ kwenye ibara ya (3).

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mswada wa fedha unahusu kodi na fedha za serikali.

    Tafuta →