Sura 8, Sehemu 4 · Art. 115
Idhini ya Rais na urejeshaji
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Katika kipindi cha muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada, Rais- (a) ataweka saini; au (b) ataurejesha Mswada Bungeni ili kuchunguzwa upya na Bunge huku likitilia maanani sababu alizo nazo Rais za kutouidhinisha mswada huo. (2) Iwapo Rais ataurejesha Mswada bungeni kuchunguzwa upya, Bunge kwa kuzingatia taratibu zinazofaa kama zilivyotajwa katika sehemu hii, linaweza- (a) kuurekebisha Mswada huo kwa kuangazia sababu muhimu alizotoa Rais; au (b) kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila kufanya marekebisho. (3) Iwapo Bunge limerekebisha Mswada huo huku likitilia maanani kikamilifu hoja za Rais, Spika anayehusika atampelekea Rais tena ili aweke sahihi. (4) Bunge, baada ya kutilia maanani sababu za Rais,linaweza kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila marekebisho au ukiwa na marekebisho ambayo hayakuyapa nafasi kwa kikamilifu hoja za Rais kwa kura ambayo itaungwa mkono na- (a) Thuluthi mbili ya wabunge wa Baraza la Kitaifa; na (b) Thuluthi mbili ya uwakilishi katika Seneti, iwapo ni Mswada unaohitaji idhini ya Seneti. (5) Iwapo Bunge litapitisha Mswada chini ya ibara ya (4)- (a) Spika wa Bunge husika atahitajika baada ya siku saba auwakilishe tena mswada huo kwa Rais; na (b) Rais atauwekea sahihi Mswada huo katika muda wa siku saba. (6) Iwapo Rais hatauwekea sahihi Mswada huo au kuurejesha kwa wakati unaopendekezwa katika Ibara ya (1), au au aweke sahihi chini ya ibara ya (5) (b), mswada huo utachukuliwa kama ulioidhinishwa kufikia kumalizika kwa kipindi hicho.
Kwa maneno rahisi
- Ndani ya siku 14 baada ya kupokea Mswada, Rais lazima aukubali au aupeleke tena Bungeni na kutoa wasiwasi wake.
Art. 115(1)
(1) Katika kipindi cha muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada, Rais- (a) ataweka saini; au (b) ataurejesha Mswada Bungeni ili kuchunguzwa upya na Bunge huku likitilia maanani sababu alizo nazo Rais za kutouidhinisha mswada huo.
Soma kifungu kamili → - Kama Bunge likipitisha Mswada tena kwa wingi wa theluthi mbili, Rais lazima aidhinishe ndani ya siku saba.
Art. 115(4)
(4) Bunge, baada ya kutilia maanani sababu za Rais,linaweza kuupitisha Mswada huo kwa mara ya pili bila marekebisho au ukiwa na marekebisho ambayo hayakuyapa nafasi kwa kikamilifu hoja za Rais kwa kura ambayo itaungwa mkono na- (a) Thuluthi mbili ya wabunge wa Baraza la Kitaifa; na (b) Thuluthi mbili ya uwakilishi katika Seneti, iwapo ni Mswada unaohitaji idhini ya Seneti.
Soma kifungu kamili → - Kama Rais hakufanya lolote ndani ya muda huo, Mswada unachukuliwa kuwa umeidhinishwa.
Art. 115(6)
(6) Iwapo Rais hatauwekea sahihi Mswada huo au kuurejesha kwa wakati unaopendekezwa katika Ibara ya (1), au au aweke sahihi chini ya ibara ya (5) (b), mswada huo utachukuliwa kama ulioidhinishwa kufikia kumalizika kwa kipindi hicho.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Rais husaini Mswada kuwa sheria au kuurudisha Bungeni na sababu.
Art. 115(1)
(1) Katika kipindi cha muda wa siku kumi na nne baada ya kupokea Mswada, Rais- (a) ataweka saini; au (b) ataurejesha Mswada Bungeni ili kuchunguzwa upya na Bunge huku likitilia maanani sababu alizo nazo Rais za kutouidhinisha mswada huo.
Soma kifungu kamili →