Sura 8, Sehemu 4 · Art. 116
Kutekelezeka kwa sheria
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Mswada unaopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais, utachapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali kama Sheria ya Bunge katika muda wa siku saba baada ya kuidhinishwa; na (2) Kwa kuzingatia ibara ya (3), Sheria ya Bunge inaanza kutekelezwa baada ya siku ya kumi na nne za kuchapishwa kwake katika Gazeti Rasmi la Serikali isipokuwa pale ambapo Sheria yenyewe inapendekeza tarehe au wakati wa kuanza kutekelezwa kwake. (3) Sheria ya Bunge ambayo moja kwa moja inatunukia maslahi ya kifedha kwa wabunge, haitaidhinishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu wa wabunge unaofuatia. (4) ibara ya (3) haitatumika kwa maslahi walionayo wabunge wakiwa kama wananchi.
Kwa maneno rahisi
- Sheria ya Bunge huchapishwa katika Gazeti ndani ya siku saba baada ya kuidhinishwa.
Art. 116(1)
(1) Mswada unaopitishwa na Bunge na kuidhinishwa na Rais, utachapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali kama Sheria ya Bunge katika muda wa siku saba baada ya kuidhinishwa; na
Soma kifungu kamili → - Sheria huanza kutumika siku ya kumi na nne baada ya kuchapishwa isipokuwa itataja tarehe nyingine.
Art. 116(2)
(2) Kwa kuzingatia ibara ya (3), Sheria ya Bunge inaanza kutekelezwa baada ya siku ya kumi na nne za kuchapishwa kwake katika Gazeti Rasmi la Serikali isipokuwa pale ambapo Sheria yenyewe inapendekeza tarehe au wakati wa kuanza kutekelezwa kwake.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Baada ya Rais kusaini sheria, inatangazwa na kuanza kutumika karibu wiki mbili baadaye.
Art. 116(2)
(2) Kwa kuzingatia ibara ya (3), Sheria ya Bunge inaanza kutekelezwa baada ya siku ya kumi na nne za kuchapishwa kwake katika Gazeti Rasmi la Serikali isipokuwa pale ambapo Sheria yenyewe inapendekeza tarehe au wakati wa kuanza kutekelezwa kwake.
Soma kifungu kamili →