Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 5 · Art. 123

Maamuzi ya Seneti

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kwa uchaguzi, wanachama wote wa Seneti ambao walikuwa wameandikishwa
kama wapigakura katika kaunti fulani, kwa pamoja wataunda ujumbe mmoja kwa
lengo la Ibara ya (4) na mwanachama aliyechaguliwa chini ya Kifungu cha (98) (1)
  (a) atakuwa ndiye kiongozi wa ujumbe huo.
(2) Wakati Seneti itakapopigia kura kuhusiana na suala lolote isipokowa Mswada, Spika
ataamua iwapo suala hilo linaathiri au kutoathiri kaunti.
(3) Seneti inapopiga kura kuhusu suala ambalo haliathiri kaunti, kila Seneta atakuwa na
kura moja.
(4) Isipokuwa iwe vinginevyo, kama inavyoagizwa na Katiba hii, kwa suala lolote katika
Seneti linaloathiri kaunti-
  (a) kila ujumbe wa kaunti utakuwa na kura moja itakayopigwa na kiongozi wa
  ujumbe wa kaunti kwa niaba ya kaunti au, endapo hakuna kiongozi wa ujumbe huo,
  basi ipigwe na mwanachama mmoja wa ujumbe huo aliyeteuliwa na kiongozi wa
  ujumbe huo.
  (b) mtu ambaye anapiga kura kwa niaba ya ujumbe ataamua iwapo apige kura kwa
  kuunga mkono au kinyume cha suala hilo, baada ya kushauriana na wajumbe; au
  (c) suala hilo litaendelezwa iwapo litaungwa mkono na wajumbe walio wengi.
Kwa maneno rahisi
  • Seneti inapopiga kura kuhusu jambo lisiloathiri kaunti, kila seneta ana kura moja.
    Art. 123(3)

    (3) Seneti inapopiga kura kuhusu suala ambalo haliathiri kaunti, kila Seneta atakuwa na kura moja.

    Soma kifungu kamili →
  • Kwa mambo yanayoathiri kaunti, kila ujumbe wa kaunti una kura moja, na jambo hupita tu kama linaungwa mkono na wingi wa wajumbe wote wa kaunti.
    Art. 123(4)

    (4) Isipokuwa iwe vinginevyo, kama inavyoagizwa na Katiba hii, kwa suala lolote katika Seneti linaloathiri kaunti- (a) kila ujumbe wa kaunti utakuwa na kura moja itakayopigwa na kiongozi wa ujumbe wa kaunti kwa niaba ya kaunti au, endapo hakuna kiongozi wa ujumbe huo, basi ipigwe na mwanachama mmoja wa ujumbe huo aliyeteuliwa na kiongozi wa ujumbe huo. (b) mtu ambaye anapiga kura kwa niaba ya ujumbe ataamua iwapo apige kura kwa kuunga mkono au kinyume cha suala hilo, baada ya kushauriana na wajumbe; au (c) suala hilo litaendelezwa iwapo litaungwa mkono na wajumbe walio wengi.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kwa mambo kuhusu kaunti, kila kaunti katika Seneti ina kura moja.

    Tafuta →