Sura 8, Sehemu 5 · Art. 125
Uwezo wa kuitisha ushahidi
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) Bunge lolote na kamati yoyote yake, lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwa kusudi la kutoa ushahidi mbele yake; (2) Kwa lengo la ibara ya (1), Bunge na kamati yake nyingineyo ina uwezo sawa na Mahakama Kuu- (a) kuhakikisha kuhudhuria kwa mashahidi na kuwahoji chini ya kiapo, kuthibitisha au vinginevyo; (b) kushurutisha utoaji wa nyaraka; na (c) kutoa agizo au ombi la kuwahoji mashahidi walio katika mataifa ya nje.
Kwa maneno rahisi
- Bunge na kamati zake zinaweza kumwita mtu yeyote kutoa ushahidi au taarifa.
Art. 125(1)
(1) Bunge lolote na kamati yoyote yake, lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwa kusudi la kutoa ushahidi mbele yake;
Soma kifungu kamili → - Kwa madhumuni haya, wana mamlaka sawa na Mahakama Kuu, ikiwemo kulazimisha kuletwa kwa nyaraka.
Art. 125(2)
(2) Kwa lengo la ibara ya (1), Bunge na kamati yake nyingineyo ina uwezo sawa na Mahakama Kuu- (a) kuhakikisha kuhudhuria kwa mashahidi na kuwahoji chini ya kiapo, kuthibitisha au vinginevyo; (b) kushurutisha utoaji wa nyaraka; na (c) kutoa agizo au ombi la kuwahoji mashahidi walio katika mataifa ya nje.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Bunge linaweza kuwaita watu kujibu maswali na kuleta nyaraka.
Art. 125(1)
(1) Bunge lolote na kamati yoyote yake, lina uwezo wa kumuita mtu yeyote kwa kusudi la kutoa ushahidi mbele yake;
Soma kifungu kamili →