Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 8, Sehemu 6 · Art. 127

Tume ya Huduma za Bunge

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kutabuniwa Tume ya Huduma ya Bunge.
(2) Tume hii itawahusisha-
  (a) Spika wa Baraza la Kitaifa kama mwenyekiti;
  (b) Naibu mwenyekiti aliyechaguliwa na Tume kutoka kwa wanachama walioteuliwa
  kwa mujibu wa aya (c);
  (c) wanachama saba walioteuliwa na Bunge kutoka miongoni mwa wabunge ambao-
  (i) wanne watateuliwa kwa usawa kutoka Mabunge yote mawili na chama au
  washirika katika muungano unaobuni Serikali ya kitaifa na ambao wawili
  kati yao watakuwa wanawake; na
  (ii) watatu watakuwa wameteuliwa na vyama visivyo kwenye Serikali ya taifa,
  angalau mmoja wao atateuliwa kutoka kila Bunge, na angalau mmoja wao
  atakuwa mwanamke; na
  (d) mwanamume na mwanamke walioteuliwa na Bunge kutoka miongoni mwa watu
  ambao si wabunge lakini wana uzoefu mkubwa katika masuala yanayohusu umma.
(3) Karani wa Seneti atakuwa katibu wa Tume hiyo.
(4) Mwanachama wa Tume atatoka afisini-
  (a) iwapo mtu huyo ni Mbunge-
  (i) baada ya kukamilika kwa kipindi cha Bunge ambacho mtu huyo alikuwa
  mbuge;
  (ii) iwapo mtu huyo anakoma kuwa Mbunge; au
  (b) iwapo mtu huyo ni mbunge mteule, baada ya kufutiliwa mbali kwa uteuzi wake
  na Bunge.
(5) licha yai Ibara ya (3), baada ya kumalizika kwa kipindi cha Bunge, mwanachama
wa Tume aliyeteuliwa kwa mujibu wa ibara ya (2) (c) ataendelea kuwa afisini hadi
mwanachama mwingine atakapoteuliwa na Bunge ili kuchukua nafasi yake.
(6) Tume ina jukumu la-
  (a) kutoa huduma na kusaidia ili kufanikisha utendakazi bora wa Bunge;
  (b) kubuni afisi katika huduma ya Bunge, na kuteua na kuwasimamia wanaoshikilia
  nyadhifa afisini humo;
  (c) kutayarisha makadirio ya matumizi ya fedha za kila mwaka katika huduma za
  Baraza la Kitaifa na kudhibiti bajeti yake;
  (d) kuanzisha ama kibinafsi au kwa pamoja na mashirika husika, mipango ya kukuza
  maadili ya demokrasia ya Bunge; na
  (e) kutekeleza majukumu mengine-
  (i) muhimu kwa manufaa ya wabunge na wafanyakazi wa Bunge; au
  (ii) yatakayopendekezwa na sheria ya kitaifa.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna Tume ya Huduma za Bunge.
    Art. 127(1)

    (1) Kutabuniwa Tume ya Huduma ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →
  • Hutoa huduma na vifaa kwa Bunge, huteua wafanyakazi wa Bunge, na huandaa bajeti ya Bunge.
    Art. 127(6)

    (6) Tume ina jukumu la- (a) kutoa huduma na kusaidia ili kufanikisha utendakazi bora wa Bunge; (b) kubuni afisi katika huduma ya Bunge, na kuteua na kuwasimamia wanaoshikilia nyadhifa afisini humo; (c) kutayarisha makadirio ya matumizi ya fedha za kila mwaka katika huduma za Baraza la Kitaifa na kudhibiti bajeti yake; (d) kuanzisha ama kibinafsi au kwa pamoja na mashirika husika, mipango ya kukuza maadili ya demokrasia ya Bunge; na (e) kutekeleza majukumu mengine- (i) muhimu kwa manufaa ya wabunge na wafanyakazi wa Bunge; au (ii) yatakayopendekezwa na sheria ya kitaifa.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Tume maalum hutunza wafanyakazi, huduma na bajeti ya Bunge.
    Art. 127(6)

    (6) Tume ina jukumu la- (a) kutoa huduma na kusaidia ili kufanikisha utendakazi bora wa Bunge; (b) kubuni afisi katika huduma ya Bunge, na kuteua na kuwasimamia wanaoshikilia nyadhifa afisini humo; (c) kutayarisha makadirio ya matumizi ya fedha za kila mwaka katika huduma za Baraza la Kitaifa na kudhibiti bajeti yake; (d) kuanzisha ama kibinafsi au kwa pamoja na mashirika husika, mipango ya kukuza maadili ya demokrasia ya Bunge; na (e) kutekeleza majukumu mengine- (i) muhimu kwa manufaa ya wabunge na wafanyakazi wa Bunge; au (ii) yatakayopendekezwa na sheria ya kitaifa.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →