Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 132

Majukumu ya Rais

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Rais ata-
  (a) toa hotuba katika ufunguzi wa kila Bunge jipya lililoteuliwa;
  (b) toa hotuba katika kikao maalumu cha Bunge mara moja kwa mwaka na anaweza
  kuhutubia Bunge wakati mwingine wowote.
  (c) Mara moja kila mwaka-
  (i) atoe ripoti, kupitia kwa hotuba kwa taifa, kuhusu hatua ambazo
  zimechukuliwa na maendeleo ambayo yamepatikana ili kufikia uadilifu wa
  kitaifa uliotajwa katika Kifungu cha cha 10;
  (ii) kuchapisha katika Gazeti Rasmi la Serikali, yaliyomo katika hatua na
  maendeleo yaliyoelezewa katika sehemu ya aya (i); na
  (iii) kuwasilisha ripoti kwa Baraza la Kitaifa ili kujadiliwa kuhusu mafanikio
  ambayo yamepatika katika utimizaji wa majukumu ya kimataifa ya Jamhuri.
(2) Rais atapendekeza na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, ateue na anaweza
kuwaachisha kazi-
  (a) Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 152;
  (b) Mwanasheria Mkuu kwa mujibu wa Kifungu cha 156;
  (c) Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 154;
  (d) Makatibu wakuu kwa mujibu wa Kifungu cha 155;
  (e) Mabalozi, wanadiplomasia, maafisa wa balozi na wawakilishi wengine wa nchi;
  na
  (f) Kwa mujibu wa Katiba hii, afisa yeyote mwingine wa taifa au wa umma ambaye
  Katiba hii inamtaka au kumpa Rais uwezo wa kumteua au kumwachisha kazi.
(3) Rais-
  (a) ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri;
  (b) ataelekeza na kuratibu majukumu ya wizara na idara za serikali; na
  (c) kwa uamuzi uliochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali, atagawa majukumu
  kwa Mawaziri ili kutekeleza na kutawala Sheria yoyote ya Bunge na si kwa kiasi
  ambacho hakiambatani na Sheria yoyote ya Bunge.
(4) Rais anaweza-
  (a) kutekeleza jukumu lolote la kiserikali lililoelekezwa katika Katiba hii au katika
  sheria ya kitaifa na, isipokuwa vinginevyo, kama ilivyoelekezwa katika, Katiba hii
  kubuni afisi katika huduma ya umma kwa mapendekezo ya Tume ya Huduma ya
  Umma;
  (b) kupokea mabalozi na wawakilishi wa balozi za nchi za nje;
  (c) kutunukia heshima kwa jina la watu na Jamhuri;
  (d) kulingana na Kifungu cha 58, kutangaza hali ya hatari; na
  (e) kwa idhini ya Bunge, anaweza kurangaza vita.
(5) Rais atahakikisha kwamba majukumu ya kimataifa kwa Jamhuri yanatimizwa kupitia
kwa utendaji wa Mawaziri husika.
Kwa maneno rahisi
  • Rais huzungumza wakati wa ufunguzi wa Bunge jipya lililochaguliwa.
    Art. 132(1)(a)

    (a) toa hotuba katika ufunguzi wa kila Bunge jipya lililoteuliwa;

    Soma kifungu kamili →
  • Rais huteua, na kwa idhini ya Bunge la Kitaifa huteua, Makatibu wa Baraza la Mawaziri na maafisa wengine wakuu.
    Art. 132(2)

    (2) Rais atapendekeza na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, ateue na anaweza kuwaachisha kazi- (a) Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 152; (b) Mwanasheria Mkuu kwa mujibu wa Kifungu cha 156; (c) Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 154; (d) Makatibu wakuu kwa mujibu wa Kifungu cha 155; (e) Mabalozi, wanadiplomasia, maafisa wa balozi na wawakilishi wengine wa nchi; na (f) Kwa mujibu wa Katiba hii, afisa yeyote mwingine wa taifa au wa umma ambaye Katiba hii inamtaka au kumpa Rais uwezo wa kumteua au kumwachisha kazi.

    Soma kifungu kamili →
  • Rais huongoza vikao vya Baraza la Mawaziri na kuelekeza shughuli za wizara.
    Art. 132(3)

    (3) Rais- (a) ataongoza mikutano ya Baraza la Mawaziri; (b) ataelekeza na kuratibu majukumu ya wizara na idara za serikali; na (c) kwa uamuzi uliochapishwa katika Gazeti Rasmi la Serikali, atagawa majukumu kwa Mawaziri ili kutekeleza na kutawala Sheria yoyote ya Bunge na si kwa kiasi ambacho hakiambatani na Sheria yoyote ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Rais huteua mawaziri (kwa idhini ya Bunge) na huongoza Baraza la Mawaziri.
    Art. 132(2)

    (2) Rais atapendekeza na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa, ateue na anaweza kuwaachisha kazi- (a) Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 152; (b) Mwanasheria Mkuu kwa mujibu wa Kifungu cha 156; (c) Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa mujibu wa Kifungu cha 154; (d) Makatibu wakuu kwa mujibu wa Kifungu cha 155; (e) Mabalozi, wanadiplomasia, maafisa wa balozi na wawakilishi wengine wa nchi; na (f) Kwa mujibu wa Katiba hii, afisa yeyote mwingine wa taifa au wa umma ambaye Katiba hii inamtaka au kumpa Rais uwezo wa kumteua au kumwachisha kazi.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →