Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 133

Mamlaka ya Huruma ya Rais

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kwa ombi la mtu yeyote, Rais anaweza kutekeleza mamlaka yake ya msamaha kwa
mujibu wa ushauri kutoka kwa Kamati ya Ushauri iliyoundwa katika Kifungu cha
(2) , kwa-
  (a) Kumsamehe kabisa au kwa masharti mtu ambaye amepatikana na hatia;
  (b) kuahirisha utekelezaji wa adhabu kwa muda uliowekwa au kwa muda
  usiojulikana;
  (c) Kubadili adhabu isiwe kali; au
  (d) Kusamehe sehemu ya adhabu au adhabu yote.
(2) Kutakuwepo na Kamati ya Ushauri kuhusu Mamlaka ya Msamaha wa Rais,
itakayowahusisha-
  (a) Mwanasheria Mkuu;
  (b) Waziri anayehusika na Huduma za Urekebishaji; na
  (c) Angalau watu wengine watano,na wasiwe watu walio kwenye huduma ya umma
  au afisi za Serikali kama inavyoidhinishwa na Sheria ya Bunge.
(3) Bunge litatunga Sheria ili kubainisha-
  (a) hatamu ya wanachama wa Kamati ya Ushauri;
  (b) Taratibu za Kamati ya Ushauri; na
  (c) Kigezo ambacho kitatumiwa na Kamati ya Ushauri katika kuunda ushauri wake.
(4) Kamati ya Ushauri inaweza kutilia maanani maoni ya waathiriwa wa hatia kuhusu
yale inayompendekezea Rais.
Kwa maneno rahisi
  • Kwa ombi la mtu, Rais anaweza kutoa msamaha, kuahirisha adhabu, kubadilisha kwa adhabu nyepesi, au kuondoa sehemu ya adhabu.
    Art. 133(1)

    (1) Kwa ombi la mtu yeyote, Rais anaweza kutekeleza mamlaka yake ya msamaha kwa mujibu wa ushauri kutoka kwa Kamati ya Ushauri iliyoundwa katika Kifungu cha

    Soma kifungu kamili →
  • Kuna Kamati ya Ushauri ya Uwezo wa Msamaha kumshauri Rais.
    Art. 133(2)

    (2) , kwa- (a) Kumsamehe kabisa au kwa masharti mtu ambaye amepatikana na hatia; (b) kuahirisha utekelezaji wa adhabu kwa muda uliowekwa au kwa muda usiojulikana; (c) Kubadili adhabu isiwe kali; au (d) Kusamehe sehemu ya adhabu au adhabu yote.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Rais anaweza kusamehe au kupunguza adhabu, kwa ushauri wa kamati maalum.
    Art. 133(1)

    (1) Kwa ombi la mtu yeyote, Rais anaweza kutekeleza mamlaka yake ya msamaha kwa mujibu wa ushauri kutoka kwa Kamati ya Ushauri iliyoundwa katika Kifungu cha

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →