Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 139

Kifo kabla ya kuchukua mamlaka

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Iwapo aliyetangazwa kuwa Rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za
uongozi-
  (a) Naibu wa rais-mteule ataapishwa kama kaimu Rais siku ileile tu ambayo Rais
  mteule angeapishwa; na
  (b) uchaguzi mpya wa Rais utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha
  Rais -Mteule.
(2) Iwapo Naibu wa rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za uongozi, afisi ya
Naibu wa rais itatangazwa kuwa wazi baada ya Rais-mteule kuchukua mamlaka.
(3) Iwapo Rais mteule pamoja na Naibu wa rais watafariki kabla ya kuchukua mamlaka-
  (a) Spika wa Baraza la Kitaifa atakuwa kaimu Rais kuanzia siku ambayo Rais mteule
  angeapishwa;na
  (b) uchaguzi mpya utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha pili.
Kwa maneno rahisi
  • Kama Rais aliyechaguliwa akifa kabla ya kuchukua madaraka, Naibu wa Rais aliyechaguliwa huapishwa kama Rais wa mpito, na uchaguzi mpya hufanyika ndani ya siku 60.
    Art. 139(1)

    (1) Iwapo aliyetangazwa kuwa Rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za uongozi- (a) Naibu wa rais-mteule ataapishwa kama kaimu Rais siku ileile tu ambayo Rais mteule angeapishwa; na (b) uchaguzi mpya wa Rais utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha Rais -Mteule.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama Rais aliyechaguliwa akifa kabla ya kuchukua madaraka, Naibu anachukua nafasi na uchaguzi mpya hufanyika.
    Art. 139(1)

    (1) Iwapo aliyetangazwa kuwa Rais-mteule atafariki kabla ya kuchukua hatamu za uongozi- (a) Naibu wa rais-mteule ataapishwa kama kaimu Rais siku ileile tu ambayo Rais mteule angeapishwa; na (b) uchaguzi mpya wa Rais utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya kifo cha Rais -Mteule.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →