Sura 9, Sehemu 2 · Art. 141
Kuchukua hatamu za Urais
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) kuapishwa kwa Rais Mteule kutafanyika wazi na mbele ya Jaji Mkuu na ikiwa Jaji Mkuu hayupo, basi mbele ya Naibu jaji mkuu. (2) Rais Mteule ataapishwa Jumanne ya kwanza itakayofuata- (a) siku kumi na nne baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Urais isipokuwa matangazo hayo yawe yamepingwa kulingana na Kifungu cha 140; ama (b) siku ya saba kufuatia tarehe ambayo mahakama inatoa uamuzi na kutangaza kuwa uchaguzi ulikuwa halali, ikiwa malalamiko yoyote yalikuwa yamewasilishwa chini ya Kifungu cha 140. (3) Rais Mteule anachukua hatamu za Urais kwa kuchukua na kutia sahihi kiapo cha uaminifu; na kiapo cha kutekeleza majukumu ya Urais kama ilivyoamriwa katika Ratiba ya Tatu. (4) Bunge kupitia kwa sheria itatoa taratibu za sherehe za kuapishwa kwa Rais-mteule.
Kwa maneno rahisi
- Kuapishwa kwa Rais aliyechaguliwa hufanyika hadharani mbele ya Jaji Mkuu au, bila yeye, Naibu Jaji Mkuu.
Art. 141(1)
(1) kuapishwa kwa Rais Mteule kutafanyika wazi na mbele ya Jaji Mkuu na ikiwa Jaji Mkuu hayupo, basi mbele ya Naibu jaji mkuu.
Soma kifungu kamili → - Rais aliyechaguliwa huchukua madaraka kwa kuapa kiapo cha uaminifu na kiapo cha kutekeleza majukumu ya ofisi.
Art. 141(3)
(3) Rais Mteule anachukua hatamu za Urais kwa kuchukua na kutia sahihi kiapo cha uaminifu; na kiapo cha kutekeleza majukumu ya Urais kama ilivyoamriwa katika Ratiba ya Tatu.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Rais mpya huapishwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu.
Art. 141(1)
(1) kuapishwa kwa Rais Mteule kutafanyika wazi na mbele ya Jaji Mkuu na ikiwa Jaji Mkuu hayupo, basi mbele ya Naibu jaji mkuu.
Soma kifungu kamili →