Sura 9, Sehemu 2 · Art. 143
Kulindwa dhidi ya kufunguliwa mashtaka.
2010-as-amended · effective 2010-08-27
Nakala halisi
(1) mashtaka yoyote ya jinai hayatafunguliwa au kuendeshwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote ambaye anashikilia afisi ya Rais wakati wa hatamu ya uongozi wake. (2) Mashtaka ya kesi za madai hayatawasilishwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote anayetekeleza majukumu ya afisi hiyo wakati wa hatamu yake kutokana na chochote anachokifanya au kutofanya katika kutekeleza mamlaka yake yaliyo kwenye Katiba hii. (3) Pale ambapo masharti katika sheria yanawekewa mipaka ya wakati ambao mashtaka haya yanaweza kuwasilishwa dhidi ya mtu huyu kwa mujibu wa Ibara ya (1) au (2), wakati ambapo mtu huyu anashikilia au kutekeleza majukumu ya afisi ya Rais hakitazingatiwa katika kuhesabu wakati ambao unaelezewa na sheria hii. (4) Kinga dhidi ya kushtakiwa kwa Rais iliyo katika Kifungu cha hiki, haitatumika kwa hatia ambazo Rais anaweza kushtakiwa chini ya mkataba wowote ambao Kenya ni mshiriki na ambao unapinga kinga kama hii.
Kwa maneno rahisi
- Kesi za jinai haziwezi kuanzishwa au kuendelea dhidi ya Rais akiwa madarakani.
Art. 143(1)
(1) mashtaka yoyote ya jinai hayatafunguliwa au kuendeshwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote ambaye anashikilia afisi ya Rais wakati wa hatamu ya uongozi wake.
Soma kifungu kamili → - Kesi za madai haziwezi kuanzishwa dhidi ya Rais akiwa madarakani kwa jambo lolote alilofanya katika kutekeleza mamlaka yake.
Art. 143(2)
(2) Mashtaka ya kesi za madai hayatawasilishwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote anayetekeleza majukumu ya afisi hiyo wakati wa hatamu yake kutokana na chochote anachokifanya au kutofanya katika kutekeleza mamlaka yake yaliyo kwenye Katiba hii.
Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
- Akiwa madarakani, Rais hawezi kufikishwa mahakamani kwa kufanya kazi yake.
Art. 143(1)
(1) mashtaka yoyote ya jinai hayatafunguliwa au kuendeshwa katika mahakama yoyote dhidi ya Rais au yeyote ambaye anashikilia afisi ya Rais wakati wa hatamu ya uongozi wake.
Soma kifungu kamili →