Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 146

Nafasi ya kazi katika afisi ya Rais

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Afisi ya Rais itakuwa wazi iwapo mwenye afisi hiyo-
  (a) Amefariki;
  (b) amejiuzulu kwa kumwandikia barua Spika wa Baraza la Kitaifa; au
  (c) ama anawacha kuwa mamlakani kwa mujibu wa Kifungu cha 144 au 145, au
  masharti mengineyo ya Katiba hii.
(2) Pale ambapo nafasi ya kazi katika afisi ya Rais itakapotokea-
  (a) Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais kwa muda uliosalia wa kipindi cha
  Rais; au
  (b) iwapo afisi ya Naibu wa rais ni wazi au Naibu wa rais hawezi kuchukua mamlaka
  ya Rais, Spika wa Baraza la Kitaifa atakuwa kaimu wa Rais na uchaguzi utafanyika
  katika muda wa siku sitini baada ya nafasi hiyo kutokea katika afisi ya Rais.
(3) Mtu anayechukua hatamu za uongozi kama Rais chini ya ibara ya (2) (a) au kufuatia
uchaguzi unaoidhinishwa na ibara ya (2) (b), isipokuwa aondolewe mamlakani kwa
mujibu wa Katiba hii, ataendelea na wadhifa huo mpaka uchaguzi mpya ufanyike
na Rais aliyechaguliwa upya kuapishwa kufuatia uchaguzi unaofuatia kwa wakati
uliowekwa wa kawaida ulio chini ya Kifungu cha 136 (1).
(4) Iwapo Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais chini ya ibara ya (2) (a) au mtu
anachaguliwa kwa afisi ya Rais chini ya Ibara ya (2) (b), Naibu wa rais au mtu yule
aliyechaguliwa watachukuliwa kufuatia kifungu cha 142 (2) kuwa-
  (a) wamehudumu kipindi kizima kama Rais, iwapo kufikia tarehe ya kuchukua
  mamlaka ya afisi, kumesalia muda wa zaidi ya miaka miwili unusu kabla ya tarehe
  ya uchaguzi utakaofuata ambao umeratibiwa chini ya Kifungu cha 136 (2) (a); au
  (b) hawajahudumu kipindi kizima kama Rais kwa hali nyingine yoyote.
Kwa maneno rahisi
  • Ofisi ya Rais inakuwa wazi kama Rais akifa, akijiuzulu, au akiacha kushikilia madaraka.
    Art. 146(1)

    (1) Afisi ya Rais itakuwa wazi iwapo mwenye afisi hiyo- (a) Amefariki; (b) amejiuzulu kwa kumwandikia barua Spika wa Baraza la Kitaifa; au (c) ama anawacha kuwa mamlakani kwa mujibu wa Kifungu cha 144 au 145, au masharti mengineyo ya Katiba hii.

    Soma kifungu kamili →
  • Kama nafasi inatokea, Naibu wa Rais huchukua madaraka kama Rais kwa kipindi kilichosalia.
    Art. 146(2)(a)

    (a) Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais kwa muda uliosalia wa kipindi cha Rais; au

    Soma kifungu kamili →
  • Kama hakuna Naibu wa Rais, Spika wa Bunge la Kitaifa hufanya kazi kama Rais na uchaguzi hufanyika ndani ya siku 60.
    Art. 146(2)(b)

    (b) iwapo afisi ya Naibu wa rais ni wazi au Naibu wa rais hawezi kuchukua mamlaka ya Rais, Spika wa Baraza la Kitaifa atakuwa kaimu wa Rais na uchaguzi utafanyika katika muda wa siku sitini baada ya nafasi hiyo kutokea katika afisi ya Rais.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama Rais anaondoka madarakani, Naibu wa Rais anachukua nafasi.
    Art. 146(2)(a)

    (a) Naibu wa rais atachukua mamlaka kama Rais kwa muda uliosalia wa kipindi cha Rais; au

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →