Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 147

Majukumu ya Naibu wa rais

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Naibu wa rais atakuwa msaidizi mkuu wa Rais na atakuwa kaimu Rais katika
utekelezaji wa majukumu ya Rais.
(2) Naibu wa rais atatekeleza majukumu yaliyotunukiwa kwake na Katiba hii na
majukumu mengine yoyote ya Rais anayoweza kupewa na Rais mwenyewe.
(3) kwa kutegemea Kifungu cha 134, wakati Rais hayupo au hawezi kutekeleza
majukumu yake kwa muda mfupi na katika kipindi kingine chochote ambacho Rais
anaweza kuamua, Naibu wa rais atakuwa kaimu wa Rais.
(4) Naibu hatashikilia mamlaka ya afisi nyingine ya Serikali au umma.
Kwa maneno rahisi
  • Naibu wa Rais ni msaidizi mkuu wa Rais na hufanya kazi za Rais bila yeye.
    Art. 147(1)

    (1) Naibu wa rais atakuwa msaidizi mkuu wa Rais na atakuwa kaimu Rais katika utekelezaji wa majukumu ya Rais.

    Soma kifungu kamili →
  • Rais akiwa hayupo au hawezi kwa muda, Naibu wa Rais hufanya kazi kama Rais.
    Art. 147(3)

    (3) kwa kutegemea Kifungu cha 134, wakati Rais hayupo au hawezi kutekeleza majukumu yake kwa muda mfupi na katika kipindi kingine chochote ambacho Rais anaweza kuamua, Naibu wa rais atakuwa kaimu wa Rais.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Naibu wa Rais humsaidia Rais na hufanya kazi Rais akiwa hayupo.
    Art. 147(1)

    (1) Naibu wa rais atakuwa msaidizi mkuu wa Rais na atakuwa kaimu Rais katika utekelezaji wa majukumu ya Rais.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →