Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 2 · Art. 149

Nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kutokea nafasi ya kazi katika afisi ya
Naibu wa rais, Rais atamteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo, nalo Baraza la
Kitaifa litapiga kura ya uamuzi wa uteuzi huo katika muda wa siku sitini baada ya
kuupokea.
(2) Iwapo mtu atachukua mamlaka ya Naibu wa rais chini ya ibara ya (1), basi kwa
kusudi la Kifungu cha 148 (8), mtu huyo atachukuliwa-
  (a) kama aliyehudumu kipindi chote cha Naibu wa rais, iwapo mnamo tarehe ya
  kuchukua mamlaka, zaidi ya miaka miwili na nusu inasalia kabla ya uchaguzi
  unaofuatia ulioratibiwa chini ya Kifungu 136 (2); au
  (b) hajahudumu katika kipindi cha afisi ya Naibu wa rais katika hali yoyote nyingine.
Kwa maneno rahisi
  • Ndani ya siku 14 baada ya nafasi ya Naibu wa Rais kutokea, Rais huteua mtu, na Bunge la Kitaifa hupiga kura ndani ya siku 60.
    Art. 149(1)

    (1) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kutokea nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais, Rais atamteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo, nalo Baraza la Kitaifa litapiga kura ya uamuzi wa uteuzi huo katika muda wa siku sitini baada ya kuupokea.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Kama Naibu wa Rais anaondoka, Rais huchagua mwingine na Bunge huthibitisha.
    Art. 149(1)

    (1) katika muda wa siku kumi na nne baada ya kutokea nafasi ya kazi katika afisi ya Naibu wa rais, Rais atamteua mtu mwingine kujaza nafasi hiyo, nalo Baraza la Kitaifa litapiga kura ya uamuzi wa uteuzi huo katika muda wa siku sitini baada ya kuupokea.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →