Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 3 · Art. 152

Baraza la Mawaziri

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Baraza la Mawaziri litakuwa na-
  (a) Rais;
  (b) Naibu wa rais;
  (c) Mwanasheria Mkuu;
  (d) Mawaziri wasiopungua kumi na wanne au kuzidi ishirini na wawili;
(2) Rais atawapendekeza na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa kuwateua Mawaziri.
(3) Waziri hatakuwa Mbunge.
(4) Kila mtu atakayeteuliwa kama waziri- atachukua mamlaka kwa kuapa au kukiri kwa
watu na Jamhuri ya Kenya na kutii Katiba, mbele ya Rais na kwa mujibu wa Ratiba
ya Nne; na anaweza kujiuzulu kwa kuwasilisha kwa Rais taarifa iliyoandikwa ya
kujiuzulu kwake.
(5) Rais –
  (a) anaweza kubadilisha kazi ya Waziri;
  (b) anaweza kumwachiza kazicWaziri; na
  (c) atamwachisha kazi waziri iwapo itahitajika kufanya hivyo, kwa uamuzi
  unaochukuliwa chini ya ibara ya (6) hadi (10).
(6) Mwanachama wa Baraza la Kitaifa anayeungwa mkono na angalau robo moja ya
wabunge wote, anaweza kupendekeza mjadala wa kumtaka Rais amwachishe kazi
waziri-
  (a) kwa misingi ya kukiuka kwa hali ya juu Vifungu vya Katiba hii au sheria
  nyingine yoyote;
  (b) kwa kuwa kuna sababu kali za kuamini kwamba Waziri amefanya kosa la jinai
  chini ya sheria za kitaifa na kimataifa; au
  (c) kwa kuwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu;
(7) Iwapo mjadala chini ya ibara ya (5) utaungwa mkono na angalau thuluthi moja ya
wabunge wote wa Baraza la Kitaifa-
  (a) Bunge litateua kamati maalumu itakayokuwa na wanachama kumi na mmoja
  kuchunguza suala hili; na
  (b) katika muda wa siku kumi, kamati hii maalumu itaripoti kwa Baraza la kitaifa
  ikiwa limepata iwapo madai dhidi ya Waziri ni ya kuthibitika.
(8) Waziri ana haki ya kwenda au kuwakilishwa mbele ya kamati maalumu wakati wa
uchunguzi wake.
(9) Iwapo kamati maalumu itaripoti kwamba imepata madai-
  (a) hayathibitiki, hakuna taratibu nyingine zitakazochukuliwa; ama
  (b) yamethibitika, Baraza la Kitaifa-
  (i) litampa Waziri nafasi ya kusikizwa; na
  (ii) litapiga kura kama litaidhinisha uamuzi unaomtaka Waziri kuachishwa kazi.
  Iwapo uamuzi ulio chini ya ibara ya (8) unaomtaka Rais kumwachiza kazi Waziri,
  utaungwa mkono na wingi wa wabunge wa Baraza la Kitaifa-
  (a) Spika kwa haraka atawasilisha uamuzi huu kwa Rais; na
  (b) Rais atamwachisha kazi waziri.
Kwa maneno rahisi
  • Baraza la Mawaziri linaundwa na Rais, Naibu wa Rais, Mwanasheria Mkuu na Makatibu wa Baraza la Mawaziri kati ya 14 na 22.
    Art. 152(1)

    (1) Baraza la Mawaziri litakuwa na- (a) Rais; (b) Naibu wa rais; (c) Mwanasheria Mkuu; (d) Mawaziri wasiopungua kumi na wanne au kuzidi ishirini na wawili;

    Soma kifungu kamili →
  • Katibu wa Baraza la Mawaziri hapaswi kuwa Mbunge.
    Art. 152(3)

    (3) Waziri hatakuwa Mbunge.

    Soma kifungu kamili →
  • Bunge la Kitaifa linaweza kumtaka Rais amfukuze Katibu wa Baraza la Mawaziri kwa ukiukaji mkubwa wa Katiba au sheria, kosa zito, au maovu makubwa.
    Art. 152(6)

    (6) Mwanachama wa Baraza la Kitaifa anayeungwa mkono na angalau robo moja ya wabunge wote, anaweza kupendekeza mjadala wa kumtaka Rais amwachishe kazi waziri- (a) kwa misingi ya kukiuka kwa hali ya juu Vifungu vya Katiba hii au sheria nyingine yoyote; (b) kwa kuwa kuna sababu kali za kuamini kwamba Waziri amefanya kosa la jinai chini ya sheria za kitaifa na kimataifa; au (c) kwa kuwa na utovu wa nidhamu wa hali ya juu;

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Baraza la Mawaziri linaundwa na Rais, Naibu wa Rais na mawaziri (Makatibu wa Baraza la Mawaziri).
    Art. 152(1)

    (1) Baraza la Mawaziri litakuwa na- (a) Rais; (b) Naibu wa rais; (c) Mwanasheria Mkuu; (d) Mawaziri wasiopungua kumi na wanne au kuzidi ishirini na wawili;

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →