Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 3 · Art. 154

Katibu wa Baraza la Mawaziri

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kuna afisi teule ya Katibu katika Baraza la Mawaziri ambayo ni afisi katika huduma
za umma.
(2) Katibu katika Baraza la Mawaziri-
  (a) atapendekezwa na Rais na kwa idhini ya Baraza la Kitaifa kuteuliwa na Rais; na
  (b) anaweza kuachishwa kazi na Rais.
(3) Katibu katika Baraza la Mawaziri-
  (a) atakuwa na madaraka ya afisi ya Baraza la Mawaziri;
  (b) atawajibika kulingana na maelekezo ya Baraza la Mawaziri, kwa kupanga
  shughuli na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza la Mawaziri;
  (c) atawasilisha uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa watu au mamlaka zinazofaa; na
  (c) atakuwa na majukumu kama itakavyoagizwa na Baraza la Mawaziri.
(4) Katibu katika Baraza la Mawaziri anaweza kujiuzulu kwa kutoa notisi ya maandishi
kwa Rais.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna ofisi ya Katibu wa Baraza la Mawaziri, katika huduma za umma.
    Art. 154(1)

    (1) Kuna afisi teule ya Katibu katika Baraza la Mawaziri ambayo ni afisi katika huduma za umma.

    Soma kifungu kamili →
  • Katibu huweka kumbukumbu za Baraza la Mawaziri, hupeleka maamuzi yake, na husimamia ofisi ya Baraza la Mawaziri.
    Art. 154(3)

    (3) Katibu katika Baraza la Mawaziri- (a) atakuwa na madaraka ya afisi ya Baraza la Mawaziri; (b) atawajibika kulingana na maelekezo ya Baraza la Mawaziri, kwa kupanga shughuli na kuweka kumbukumbu za mikutano ya Baraza la Mawaziri; (c) atawasilisha uamuzi wa Baraza la Mawaziri kwa watu au mamlaka zinazofaa; na (c) atakuwa na majukumu kama itakavyoagizwa na Baraza la Mawaziri.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Katibu huweka kumbukumbu za Baraza la Mawaziri na kupeleka maamuzi.

    Tafuta →