Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 4 · Art. 157

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kutabuniwa afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
(2) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atapendekezwa na Rais, na kwa idhini ya
Baraza la Kitaifa, atateuliwa na Rais.
(3) Sifa za uteuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma zitakuwa sawa na zile za
uteuzi wa Jaji wa Mahakama Kuu.
(4) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atakuwa na mamlaka ya kumwagiza Inspekta
Mkuu wa Huduma ya Polisi ya Kenya kuchunguza habari yoyote au madai ya
vitendo vya jinai, naye Inspekta Mkuu wa Huduma ya Polisi ya Kenya atatii maagizo
hayo.
(5) Mkurugenzi wa mashtaka ya Umma atashikilia hatamu ya afisi yake kwa kipindi cha
miaka nane na hatakuwa na nafasi ya kuteuliwa tena.
(6) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atatekeleza mamlaka ya Taifa ya kuongoza
mashtaka na anaweza-
  (a) Kuwasilisha na kuendeleza mashtaka ya kesi za uhalifu dhidi ya mtu yeyote
  katika mahakama yoyote (isipokuwa mahakama ya kijeshi) kutokana na kosa
  linalotuhumiwa kuwa limefanywa;
  (b) Kuchukua na kuendeleza kesi zozote ya uhalifu zilizowasilishwa katika
  mahakama yoyote (isipokuwa katika mahakama ya kijeshi) zilizowasilishwa na
  kuendelezwa na mtu mwingine au mamlaka; na
  (c) Kwa kutegemea ibara ya (7) na (8), kukomesha katika hatua yoyote, kabla ya
  hukumu kutolewa, kesi yoyote ya uhalifu iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa
  Mashtaka ya Umma au kuchukuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya umma
  kulingana na aya (b)
(7) Pale ambapo kukomeshwa kwa kesi kunakorejelewa katika ibara ya (6) (c)
kunapotekelezwa baada ya mshitakiwa kukamilisha kujitetea, mshitakiwa
ataachiliwa huru.
(8) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma hawezi kukomesha shitaka lolote bila ya idhini
ya mahakama.
(9) Mamlaka ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kuyaendesha yeye
mwenyewe ama kumuagiza afisa wa afisi yake kulingana na masharti maalum au ya
jumla.
(10) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma hatahitaji idhini ya mtu au mamlaka yoyote
kuwasilisha kesi za kijinai, na katika kutekeleza mamlaka au majukumu yake
hataelekezwa au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.
(11) Katika kutekeleza mamlaka yaliyotunukiwa na Kifungu hiki, Mkurugenzi wa
Mashtaka ya Umma atazingatia maslahi ya taifa, maslahi ya utekelezaji wa haki na
haja ya kuzuia na kuepuka matumizi mabaya ya utaratibu wa sheria.
(12) Bunge linaweza kutunga sheria ya kutunukia taasisi nyingine uwezo wa kuongoza
mashtaka kuliko ile ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
Kwa maneno rahisi
  • Kuna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
    Art. 157(1)

    (1) Kutabuniwa afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

    Soma kifungu kamili →
  • Mkurugenzi ana mamlaka ya kumwagiza Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Kitaifa kuchunguza madai yoyote ya tabia ya jinai.
    Art. 157(4)

    (4) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atakuwa na mamlaka ya kumwagiza Inspekta Mkuu wa Huduma ya Polisi ya Kenya kuchunguza habari yoyote au madai ya vitendo vya jinai, naye Inspekta Mkuu wa Huduma ya Polisi ya Kenya atatii maagizo hayo.

    Soma kifungu kamili →
  • Mkurugenzi hutumia mamlaka ya Serikali ya kushtaki na hayuko chini ya maelekezo au udhibiti wa mtu yeyote.
    Art. 157(10)

    (10) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma hatahitaji idhini ya mtu au mamlaka yoyote kuwasilisha kesi za kijinai, na katika kutekeleza mamlaka au majukumu yake hataelekezwa au kudhibitiwa na mtu au mamlaka yoyote.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mkurugenzi huamua nani anafikishwa mahakamani kwa makosa, na hufanya kazi kwa uhuru.
    Art. 157(6)

    (6) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma atatekeleza mamlaka ya Taifa ya kuongoza mashtaka na anaweza- (a) Kuwasilisha na kuendeleza mashtaka ya kesi za uhalifu dhidi ya mtu yeyote katika mahakama yoyote (isipokuwa mahakama ya kijeshi) kutokana na kosa linalotuhumiwa kuwa limefanywa; (b) Kuchukua na kuendeleza kesi zozote ya uhalifu zilizowasilishwa katika mahakama yoyote (isipokuwa katika mahakama ya kijeshi) zilizowasilishwa na kuendelezwa na mtu mwingine au mamlaka; na (c) Kwa kutegemea ibara ya (7) na (8), kukomesha katika hatua yoyote, kabla ya hukumu kutolewa, kesi yoyote ya uhalifu iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma au kuchukuliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya umma kulingana na aya (b)

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →