Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 9, Sehemu 4 · Art. 158

Kuondolewa na Kujiuzulu kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kuachishwa kazi tu kwa misingi ya-
  (a) kutoweza kutekeleza majukumu ya afisi kutokana na kukosa uwezo wa kiakili au
  wa kimwili;
  (b) kutozingatia Sura ya Sita.
  (c) kufilisika
  (d) kutokuwa na umilisi.
  (e) utovu wa nidhamu na tabia mbaya
(2) Mtu anayetaka kuondolewa mamlakani kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umm,
anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Huduma ya Umma ambayo,
itakuwa kwa maandishi yakidhihirisha uhakika wa madai yanayounda msingi wa
kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.
(3) Tume ya Huduma ya Umma itaangalia malalamiko haya na, ikiridhika kwamba
yanafichua kwa msingi wa malalamiko chini ya Ibara ya (1), itapeleka malalamiko
haya kwa Rais.
(4) Baada ya kuyapokea na kuyachunguza malalamiko haya, Rais, kwa muda wa siku
kumi na nne, atamsimamisha kazi Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ikisubiriwa
uamuzi wa Rais kulingana na ibara ya (5) na atatekeleza haya kulingana na ushauri
wa Tume ya Huduma ya Umma, atateua tume maalum itakayokuwa na-
  (a) wanachama wanne kutoka miongoni mwa wale ambao wanashikilia au
  wameshawahi kushikilia afisi kama jaji wa mahakama yenye mamlaka makuu, au
  wale ambao wamehitimu kuweza kuteuliwa kwa afisi kama hii ;
  (b) wakili mmoja ambaye amehudumu kwa angalau miaka kumi na mitano na
  atakayeteuliwa na taasisi ya kisheria inayowajibika kuthibiti taaluma ya uwakili; na
  (c) watu wengine wawili walio na uzoefu wa masuala ya umma.
(5) Kamati itachunguza suala hilo kikamilifu na kuripoti kuhusu ukweli huo na kutoa
mapendekezo kwa Rais ambaye atachukua hatua kulingana na mapendekezo hayo ya
tume maalum.
(6) Mkurugezi wa Mashtaka ya Umma, ambaye amesimamishwa kazi kulingana na ibara
ya (4) atapokea nusu ya mshahara hadi wakati wa kuachishwa kazi au kurudishwa
kazini.
(7) Tume Maalum iliyoteuliwa kulingana na ibara ya (4) itamchagua mwenyekiti
miongoni mwao.
(8) Tume Maalum iliyochaguliwa kulingana na ibara ya (4) itawajibika kuthibiti taratibu
zake.
(9) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kujiuzulu kwa kumuandikia barua
Rais.
Kwa maneno rahisi
  • Mkurugenzi anaweza kuondolewa tu kwa kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi, kutofuata Sura ya Sita, kufilisika, kukosa umahiri, au maovu makubwa.
    Art. 158(1)

    (1) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kuachishwa kazi tu kwa misingi ya- (a) kutoweza kutekeleza majukumu ya afisi kutokana na kukosa uwezo wa kiakili au wa kimwili; (b) kutozingatia Sura ya Sita. (c) kufilisika (d) kutokuwa na umilisi. (e) utovu wa nidhamu na tabia mbaya

    Soma kifungu kamili →
  • Mtu anayetaka kuondolewa huwasilisha ombi kwa Tume ya Huduma za Umma.
    Art. 158(2)

    (2) Mtu anayetaka kuondolewa mamlakani kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umm, anaweza kuwasilisha malalamiko yake kwa Tume ya Huduma ya Umma ambayo, itakuwa kwa maandishi yakidhihirisha uhakika wa madai yanayounda msingi wa kuondolewa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma.

    Soma kifungu kamili →
  • Mkurugenzi anaweza kujiuzulu kwa kutoa taarifa kwa maandishi kwa Rais.
    Art. 158(9)

    (9) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kujiuzulu kwa kumuandikia barua Rais.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mkurugenzi anaweza kuondolewa kwa sababu kubwa tu, kwa mchakato mkali.
    Art. 158(1)

    (1) Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma anaweza kuachishwa kazi tu kwa misingi ya- (a) kutoweza kutekeleza majukumu ya afisi kutokana na kukosa uwezo wa kiakili au wa kimwili; (b) kutozingatia Sura ya Sita. (c) kufilisika (d) kutokuwa na umilisi. (e) utovu wa nidhamu na tabia mbaya

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →