Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 10, Sehemu 2 · Art. 164

Mahakama ya Rufani

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Kutabuniwa Mahakama ya Rufaa, ambayo –
  (a) itakuwa na idadi ya majaji ambao hawatapungua kumi na wawili kulingana na
  sheria za bunge; na
  (b) inaundwa na kusimamiwa kulingana na ufafanuzi wa Sheria ya Bunge.
(2) Kutakuwa na Rais wa Mahakama ya Rufaa ambaye atachaguliwa na majaji wa
mahakama ya Rufaa kutoka miongoni mwao.
(3) Mahakama ya Rufaa ina mamlaka ya kusikiza rufaa kutoka –
  (a) Mahakama Kuu; na
  (b) mahakama nyingine au mahakama maalum kulingana na Sheria ya Bunge.
Kwa maneno rahisi
  • Mahakama ya Rufaa inaundwa na majaji wasiopungua kumi na wawili.
    Art. 164(1)

    (1) Kutabuniwa Mahakama ya Rufaa, ambayo – (a) itakuwa na idadi ya majaji ambao hawatapungua kumi na wawili kulingana na sheria za bunge; na (b) inaundwa na kusimamiwa kulingana na ufafanuzi wa Sheria ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →
  • Inasikiliza rufaa kutoka Mahakama Kuu na mahakama au baraza lingine lolote linalowekwa na Sheria ya Bunge.
    Art. 164(3)

    (3) Mahakama ya Rufaa ina mamlaka ya kusikiza rufaa kutoka – (a) Mahakama Kuu; na (b) mahakama nyingine au mahakama maalum kulingana na Sheria ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Mahakama ya Rufaa husikiliza rufaa kutoka Mahakama Kuu.
    Art. 164(3)

    (3) Mahakama ya Rufaa ina mamlaka ya kusikiza rufaa kutoka – (a) Mahakama Kuu; na (b) mahakama nyingine au mahakama maalum kulingana na Sheria ya Bunge.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →