Skip to content
KenyaSimplified

Imetafsiriwa ili kukusaidia kuelewa. Nakala rasmi ya Katiba ya Kenya ni ya Kiingereza; kama kuna tofauti yoyote, nakala ya Kiingereza ndiyo yenye nguvu. Hii si ushauri wa kisheria. Kanusho

Sura 10, Sehemu 2 · Art. 166

Uteuzi wa Jaji Mkuu, Naibu wa Jaji Mkuu na Majaji wengine

2010-as-amended · effective 2010-08-27

Nakala halisi

(1) Rais atateua-
  (a) Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu kulingana na mapendekezo ya Tume ya Huduma
  ya Mahakama na kwa idhini ya Bunge; na
  (b) majaji wengine wote, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za
  Mahakama.
(2) Majaji wa mahakama za mamlaka ya juu watateuliwa kutoka miongoni mwa watu
ambao –
  (a) wana shahada katika taaluma ya sheria kutoka chuo kinachotambulika, au ni
  mawakili wa Mahakama Kuu, au wana hitimu sawa na hizo katika masuala ya
  kawaida ya kisheria;
  (b) wana tajriba inayohitajika ambayo wameipata nchini Kenya na taasisi nyingine
  za mataifa yanayotumia mamlaka ya sheria ya Jumuia ya Madola kama zinazotajwa
  katika ibara ya (3) hadi (6); na
  (c) wana mienendo na maadili mema na hawabagui.
(3) Jaji Mkuu na majaji wa Mahakama ya Juu watateuliwa kutoka miongoni mwa watu
ambao wana –
  (a) tajriba ya miaka kumi na mitano kama jaji katika mahakama ya mamlaka ya juu;
  au
  (b) tajriba ya miaka isiyopungua kumi na mitano kama msomi anayeheshimika, afisa
  katika idara ya mahakama, uanasheria au tajriba kama hiyo katika maeneo mengine
  ya taaluma ya uanasheria; au
  (c) amehitimu kwa viwango vilivyotajwa katika aya (a) na (b) kwa jumla ya miaka
  kumi na mitano;
(4) Kila jaji wa Mahakama ya Rufaa atateuliwa kutoka miongoni mwa watu ambao
wana–
  (a) tajriba ya miaka isiyopungua kumi kama jaji wa Mahakama ya kiwango cha juu;
  au
  (b) tajriba ya miaka isiyopungua kumi kama msomi anayeheshimika au mwanasheria
  au tajriba kama hiyo katika nyanja nyingine husika ya kisheria; au
  (c) amehitimu kwa viwango vilivyotajwa katika aya (a) na (b) kwa muda wa jumla
  ya miaka kumi.
(5) Kila jaji wa Mahakama Kuu atateuliwa kutoka miongoni mwa watu walio na –
  (a) tajriba isiyopungua miaka kumi kama jaji katika mahakama ya kiwango cha juu;
  au
  (b) tajriba ya miaka isiyopungua kumi kama msomi anayeheshimika au
  mwanasheria au tajriba kama hiyo katika nyanja nyingine husika ya kisheria; au
  (c) amehitimu kwa viwango vilivyotajwa katika aya (a) na (b) kwa jumla ya muda
  wa miaka kumi.
Kwa maneno rahisi
  • Rais humteua Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu kwa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama, kwa idhini ya Bunge la Kitaifa, na huteua majaji wengine kwa mapendekezo ya Tume.
    Art. 166(1)

    (1) Rais atateua- (a) Jaji Mkuu na Naibu Jaji Mkuu kulingana na mapendekezo ya Tume ya Huduma ya Mahakama na kwa idhini ya Bunge; na (b) majaji wengine wote, kwa mujibu wa mapendekezo ya Tume ya Huduma za Mahakama.

    Soma kifungu kamili →
  • Majaji huteuliwa kutoka kwa watu walio na shahada ya sheria au mawakili, wenye uzoefu unaohitajika na tabia njema ya juu.
    Art. 166(2)

    (2) Majaji wa mahakama za mamlaka ya juu watateuliwa kutoka miongoni mwa watu ambao – (a) wana shahada katika taaluma ya sheria kutoka chuo kinachotambulika, au ni mawakili wa Mahakama Kuu, au wana hitimu sawa na hizo katika masuala ya kawaida ya kisheria; (b) wana tajriba inayohitajika ambayo wameipata nchini Kenya na taasisi nyingine za mataifa yanayotumia mamlaka ya sheria ya Jumuia ya Madola kama zinazotajwa katika ibara ya (3) hadi (6); na (c) wana mienendo na maadili mema na hawabagui.

    Soma kifungu kamili →
Maelezo ya watoto
  • Majaji huteuliwa kwa kuzingatia sifa zao na tabia njema.
    Art. 166(2)

    (2) Majaji wa mahakama za mamlaka ya juu watateuliwa kutoka miongoni mwa watu ambao – (a) wana shahada katika taaluma ya sheria kutoka chuo kinachotambulika, au ni mawakili wa Mahakama Kuu, au wana hitimu sawa na hizo katika masuala ya kawaida ya kisheria; (b) wana tajriba inayohitajika ambayo wameipata nchini Kenya na taasisi nyingine za mataifa yanayotumia mamlaka ya sheria ya Jumuia ya Madola kama zinazotajwa katika ibara ya (3) hadi (6); na (c) wana mienendo na maadili mema na hawabagui.

    Soma kifungu kamili →

    Tafuta →